Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Joseph Modest Mkude, alikuwa mgeni rasmi katika fainali ya Salumu Cup iliyofanyika Agosti 18, 2024, katika viwanja vya Badi, kata ya Mwakipoya. Fainali hiyo ilikutanisha timu mbili, Gazza FC kutoka Kishapu na Sanga Itinje FC kutoka Meatu, ambapo Gazza FC ilishinda kwa magoli 2-0.

Mhe. Mkude alizipongeza timu zote zilizoshiriki mashindano haya, akisisitiza kuwa michezo ni njia muhimu ya kukuza afya na mshikamano katika jamii. Aliwataka wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kati ya tarehe 21-27 Agosti 2024, na kujitayarisha kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, alipongeza timu zote kwa mchezo mzuri na kuahidi kuendelea kuunga mkono vijana katika masuala ya michezo.


Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa