• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

DED JOHNSON ATAKA USHIRIKIANO KUINUA ELIMU SHULE YA MSINGI NG'WANIMA

Posted on: September 4th, 2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungunza kwenye mkutano wake maalum uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, Kata ya Busangwa uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi na maendeleo ya Shule hiyo Septemba 4,2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Emmanuel Johnson, ametoa rai kwa Wazazi, Walimu na Viongozi wa Vijiji kushirikiana kwa karibu ili kuinua kiwango cha elimu kwa watoto wao, akisisitiza mshikamano kama nguzo ya maendeleo ya elimu.


Johnson ametoa kauli hiyo Septemba 3, 2025, katika mkutano uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, Kata ya Busangwa, uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi na maendeleo ya Shule hiyo.

Amesema jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kutoa fedha nyingi kwa sekta ya elimu hazina budi kuungwa mkono kwa vitendo, akibainisha kuwa serikali inaendelea kuondoa vikwazo ili watoto wote wapate elimu bora bila gharama.

“Walimu waongeze bidii katika ufundishaji, wazazi wawasiliane kwa karibu na walimu, na kamati za shule ziwe kiungo cha kuondoa changamoto zinazojitokeza. Umoja ndio silaha ya mafanikio hayo”. amesema Johnson.

 

Afisa Elimu Taaluma wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Daniel Bilole, akizungunza kwenye mkutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, Kata ya Busangwa uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi wa maendeleo ya Shule hiyo Septemba 4,2025

Aidha, amehimiza wazazi kuwaheshimu na kuwapongeza walimu kwa juhudi zao, lakini pia wasisite kuwakosoa pale panapojitokeza mapungufu.


Mkurugenzi huyo amewakumbusha Wazazi kufuatilia mienendo ya Watoto wao wanapokuwa nje ya Shule,kukagua madaftari yao,kuhoji siku yao ilivyokuwa shuleni sambamba na kuwalea katika maadili ya Ki Tanzania na kuzingatia umuhimu wa elimu kama msingi wa maisha yao ya baadaye.

“Mtoto anapofundishwa Shuleni halafu akiachiwa nje ya shule bila uangalizi, juhudi za mwalimu hubaki bure. Ushirikiano kati ya malezi ya nyumbani na elimu ya Shuleni ni jambo lisilokwepeka,” ameongeza Mkurugenzi Johnson.

Amengeza kuwa Halmashauri itaendelea kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za Walimu na miradi mingine ya elimu, huku akiomba wananchi waendelee kushirikiana na serikali kuanzisha maboma ya madarasa na majengo ya huduma za afya

ambayo baadaye serikali itayakamilisha katika hatua ya upauaji,uwekaji vifaa na usajili rasmi.

 

Mtendaji wa Kata ya Busangwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Boniphace Ngaka akizungunza kwenye mkutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi na maendeleo ya Shule hiyo Septemba 4,2025

Kwa upande wake, Afisa Elimu Taaluma wa Wilaya ya Kishapu, Daniel Bilole, amesisitiza kuwa mshikamano wa pamoja kati ya Walimu na Wazazi ndio nyenzo muhimu ya kuongeza ufaulu huku akiwapongeza waalimu kwa kuinua elimu dalasani na kwenye michezo

Wazazi walioshiriki mkutano huo akiwemo Mhangilwa Malieta, Charles Lutalenya na Lucia Ngassa, wamempongeza Mkurugenzi Johnson kwa kusogea karibu na wananchi na kusikiliza changamoto kwa uwazi, wakisema hatua hiyo imewapa hamasa mpya

ya kushirikiana katika kuinua kiwango cha elimu

  .

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ng'wanima Kata ya Busangwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Ndulu Shema akizungunza kwenye mkutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi na maendeleo ya Shule hiyo Septemba 4,2025

Mkutano huo ni sehemu ya juhudi za Halmashauri ya Kishapu kujenga uhusiano wa karibu kati ya jamii na Walimu, ikizingatiwa kuwa elimu bora haiwezi kuachwa mikononi mwa serikali peke yake.Ushirikiano wa kijamii unahitajika ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi, kupunguza changamoto za miundombinu na kuhakikisha fedha zinazotolewa na serikali zinakuwa na matokeo chanya kwa walengwa.


Kwa ujumla, hatua ya Mkurugenzi Johnson kukutana na wazazi shuleni ni mfano wa uongozi shirikishi unaolenga kuondoa pengo kati ya sera za elimu na utekelezaji wake katika ngazi ya jamii.

Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Ng'wanima Kata ya Busangwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Seni Malieta akizungunza kwenye mkutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi na maendeleo ya Shule hiyo Septemba 4,2025

 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Ng'wanima Kata ya Busangwa Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Octavian Katunzi Salvatory akizungunza kwenye mkutano wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson uliofanyika Shule ya Msingi Ng’wanima, uliowakutanisha Wazazi, Walimu, Viongozi wa Kata, Vijiji na Vitongoji kwa lengo la kujadili ustawi na maendeleo ya Shule hiyo Septemba 4,2025

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akiwa na Mwanafunzi wa darasa la saba Shule ya Msingi Ng'wanima Kata ya Busongwa Wilayani humo aliyekuwa mshindi wa kwanza mashindano ya UMITASHUMTA Tanzania na wa pili Afrika Mashariki mwaka 2025


Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MKURUGENZI JOHNSON AWATAKIA MTIHANI MWEMA WANAFUNZI WA DARASA LA SABA

    September 09, 2025
  • DED JOHNSON ATAKA USHIRIKIANO KUINUA ELIMU SHULE YA MSINGI NG'WANIMA

    September 04, 2025
  • TIP YAFANYA MAFUNZO REJEA DHIDI YA UKATILI KISHAPU

    September 03, 2025
  • DC MASINDI AWATAKA WAGOMBEA KUTUMIA LUGHA YA STAHA JUKWAANI AHITIMISHA ZIARA

    August 27, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa