• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

DED KISHAPU AHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA NGO's NA SERIKALI

Posted on: June 23rd, 2025


Mkurugenzi Mtendaji wa wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga imeyakutanisha Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali 16 (NGOs) yanayofanya kazi mbalimbali za kijamii Wilayani humo na Uongozi wa Wilaya hiyo kwa ajili ya kujadili shughuli wanazozifanya katika maeneo yao ya kazi, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazowakabili.

Akizungumza katika kikao hicho wakati wa ufunguzi Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Emmanuel Johnson ameyapongeza mashirika hayo kwa kazi kubwa wanayofanya ya kusaidia jamii kwenye afua mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo afya,maji,elimu,miundombinu, jinsia, mazingira na haki za watoto.

Johnson Amesisitiza umuhimu wa kuongea kuimarisha mahusiano ya ushirikiano baina ya mashirika hayo na ofisi za umma ambazo zitawasaidia kuwaeleza kuhusu sheria za nchi na na sera za kisekta zielekezavyo kwani hiyo itasaidia katika utekelezaji wa shughuli zao kuleta matokeo chanya zaidi.

“Tunatambua mchango wenu katika maendeleo ya wananchi wa Kishapu hivyo ni muhimu sana kushirikiana kwa karibu, kubadilishana taarifa, na kupanga kwa pamoja ili tuongeze tija.Pia nawahimiza mkipata nafasi ya fedha zaidi mpanue wigo wa miradi yenu ifike kwenye Kata na Vijiji ambavyo bado havijafikiwa na miradi hii muhimu na elimu iletayo mabadiliko ya kimtazamo” amesema Mkurugenzi Johnson.

Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ambaye pia ni Afisa Tawala ofisi ya Mkuu wa Wilaya Fadhiri Mvanga amesema serikali itaendelea kushirikiana na mashirika hayo bega kwa bega ili kuleta mabadiliko kwa wananchi na amehimiza kuendelea kutoa elimu ya kujikwamua kiuchumi hasa kwa vijana walioko migodini alimarufu "Wabeshi".

"Kuna badhi ya vijana ni wadogo kiumri lakini wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye uchimbaji na wasipate kitu nashauri ikiwezekana muwekeze pia fedha huko ili wapate elimu ya kubuni vyanzo vipya vya biashara na wajipatie kipato na hata wanaojipenyeza kinyume cha shera na taratibu za nchi" ameongeza Mvanga

Ameongeza kuwa iko sababu ya mashirika kutenga bajeti ya majanga na dharula mbalimbali ili pindi yanapotokea yasiathiri moja kwa moja fedha za miradi wanayotekeleza.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Afisa Tawala Fadhiri Mvanga akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Mwenyekiti wa mashirika Wilayani Kishapu (NaCONGO) Venas Chunga Nikombe, amesema mashirika hayo yatatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa ofisi za serikali ngazi zote pamoja na kutekeleza shughuli zao kwa weledi mkubwa kwa kuzingatia misingi ya kisheria, kanuni, taratibu na pia kuheshimu mila, desturi na utamaduni za jamii wanazozihudumia.
Katika kikao hicho, wawakilishi wa mashirika mbalimbali wamepata fursa ya kueleza shughuli walizotekeleza, maeneo wanayofanyia kazi, mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto wanazokutana nazo.

Afisa maendeleo ya jamii Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala akizungumza kwenye kikao maalumu kilichoandaliwa na Halmashauri ya Wilaya hiyo na kuwakutanisha wadau wa maendeleo Mashirika yasiyo ya kiserikali kujadili shughuli wanazozifanya na kuweka maazimio ya pamoja katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo Juni 23,2025 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Kwa upande wao, baadhi ya wawakilishi wa mashirika hayo wameeleza kufurahishwa na hatua hiyo ya uongozi wa wilaya kuwaita kwa majadiliano ya pamoja, wakisema hatua hiyo ni muhimu kwa uwazi, uelewano na kuimarisha utekelezaji wa miradi kwa tija zaidi.
Maazimio haya yanatarajiwa kuwa msingi wa kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na wadau wa maendeleo katika kuiletea jamii ya Kishapu maendeleo endelevu na jumuishi.

Kikao hicho kimejumuisha Mwenyekiti wa mashirika (NaCONGO) ngazi ya Mkoa Bw.Bakari Juma Kibile na miongoni mwa mashirika yaliyoshiriki ni pamoja na KIWOHEDE, TGNP Mtandao, SHIDEPHA+, World Vision, MEDEA, TCRS, baadhi ya wataalamu wa Halmashauri pamoja na viongozi wa mashirika kwa ngazi ya Wilaya.

Kikao hicho kimetajwa kuwa ni mwanzo mzuri wa mpango wa Halmashauri wa kuanzisha mfumo wa ufuatiliaji na uratibu wa pamoja baina ya Serikali na wadau wa maendeleo kwa lengo la kuhakikisha miradi inayotekelezwa inaleta matokeo yenye tija kwa wananchi wa Kishapu.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • VIJIJI 16 VINAVYOZUNGUKA MIGODI KISHAPU MIGOGORO YA ARDHI KUKOMESHWA

    June 27, 2025
  • TAKUKURU YAZINDUA JENGO JIPYA KISHAPU, LAWAPA WANANCHI IMANI NA UJASIRI KUPINGA RUSHWA

    June 26, 2025
  • DED KISHAPU AHIMIZA USHIRIKIANO KATI YA NGO's NA SERIKALI

    June 23, 2025
  • TIP YAENDESHA MAFUNZO YA KUPINGA UKATILI KISHAPU

    June 17, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa