• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
    • Ratiba ya vikao vya kisheria vya MSM
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

KISHAPU YAJIPANGA KUONGEZA UZALISHAJI PAMBA

Posted on: February 4th, 2026

Mwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamati ya mazao na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga, Afisa Tawala wa wilayani humo, Fadhili Joseph Mvanga akizungumza kwenye kikao maalum cha Kamati ya Mazao ya Wilaya kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU Februari 4,2026, kikilenga kusikiliza changamoto zinazokabili zao la pamba na kuweka mikakati sahihi na ya pamoja katika uboreshaji wa uzalishaji, masoko na manufaa ya moja kwa moja kwa mkulima


Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Samia Suluhu imeendelea kuchukua hatua madhubuti za kulirejesha zao la pamba katika hadhi yake ya kihistoria na kiuchumi, huku mkulima akiwekwa mbele katika mnyororo mzima wa thamani wa zao hilo, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuongeza uzalishaji wenye tija na kuinua maisha ya wakulima.


Hatua hiyo imebainishwa Februari 4, 2026 wakati wa kikao maalum cha Kamati ya Mazao Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU, kikilenga kusikiliza changamoto zinazokabili zao la pamba na kuweka mikakati sahihi na ya pamoja katika uboreshaji wa uzalishaji, masoko na manufaa ya moja kwa moja kwa mkulima.


Kikao hicho ni sehemu ya mpango wa Serikali wa kulifanya zao la pamba kuwa zao la kimkakati linalochangia kikamilifu uchumi wa mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, huku kikao hicho kikiendeshwa na mwakilishi wake, Afisa Tawala wa Wilaya ya Kishapu, Fadhili Joseph Mvanga.


Akizungumza katika kikao hicho, Mvanga amesisitiza kuwa Serikali inalenga kuimarisha mifumo ya uzalishaji, pembejeo, usimamizi na masoko ili mkulima apate faida halisi, sambamba na kurejesha imani ya wakulima katika zao la pamba.


"Ili tufikie dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya Mhe. Samia Suluhu katika kuimarisha maisha ya mkulima kupitia mazao ya kimkakati ikiwemo pamba, nihimize kuwepo ufuatiliaji wa karibu, mawasiliano ya mara kwa mara kati ya maafisa ugani na wakulima, pamoja na utoaji wa elimu kwa wakati ili kuongeza uzalishaji na ubora wa zao hilo" ameongeza Mvanga.


Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Mhe. Josephat Limbe, ameiomba Bodi ya Pamba Tanzania kuzingatia ombi la Wilaya la kuruhusu uwepo wa wanunuzi zaidi ya mmoja wa zao la pamba, hatua itakayoongeza ushindani wa masoko, kuimarisha bei na kumpa mkulima uhakika wa faida kuelekea msimu wa uzalishaji wa 2026/2027.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Marco Mtunga, ameihakikishia Wilaya ya Kishapu kuwa Serikali inaendelea kuboresha sera, usimamizi na ushirikiano na wadau ili kuimarisha soko la pamba na kuhakikisha mkulima analindwa dhidi ya changamoto za bei na masoko.


Balozi wa zao la pamba, Aggrey Mwanri, akizungumza katika kikao hicho ametoa wito kwa wadau wote kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha elimu, teknolojia na ubunifu vinatumika ipasavyo ili kulifanya zao la pamba kuwa la kisasa, lenye tija na linalomlipa mkulima stahiki yake.

Hata hivyo Wilaya ya Kishapu imebainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa mpaka sasa katika maandalizi ya msimu wa pamba, ikiwemo upatikanaji wa tani 2,555 za mbegu za pamba, viuatilifu 264,232 kati ya 840,000 vinavyotarajiwa, pamoja na mbolea hai lita 20,200 sawa na asilimia 80 ya mapipa na matenki yaliyonunuliwa na makampuni husika.


Aidha, Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya uzalishaji kwa kuwezesha trekta 19, maafisa wa mpango wa BBT 78 wakiwa na pikipiki 74, pamoja na vifaa vya kisasa vya kunyunyizia viuatilifu ikiwemo Boom Sprayers 3 na Drones 9, hatua inayolenga kuongeza ufanisi na kupunguza gharama kwa mkulima.


Kikao hicho kimehudhuriwa na wadau mbalimbali wa zao la pamba wakiwemo maafisa wa BBT, wanunuzi wa pamba, viongozi wa AMCOS, maafisa ugani na madiwani, hatua inayodhihirisha mshikamano wa pamoja katika kulijenga na kulirejesha zao la pamba kama nguzo muhimu ya uchumi wa Wilaya ya Kishapu.

Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Pamba Tanzania, Marco Mtunga akizungumza kwenye kikao maalum cha Kamati ya Mazao ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU Februari 4,2026, kikilenga kusikiliza changamoto zinazokabili zao la pamba na kuweka mikakati sahihi na ya pamoja katika uboreshaji wa uzalishaji, masoko na manufaa ya moja kwa moja kwa mkulima

Balozi wa zao la pamba, Aggrey Mwanri, akizungumza kwenye kikao maalum cha Kamati ya Mazao ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU Februari 4,2026, kikilenga kusikiliza changamoto zinazokabili zao la pamba na kuweka mikakati sahihi na ya pamoja katika uboreshaji wa uzalishaji, masoko na manufaa ya moja kwa moja kwa mkulima

Mwenyekiti wa Halmahshauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe, akizungumza kwenye kikao maalum cha Kamati ya Mazao ya wilayani humo kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU Februari 4,2026, kikilenga kusikiliza changamoto zinazokabili zao la pamba na kuweka mikakati sahihi na ya pamoja katika uboreshaji wa uzalishaji, masoko na manufaa ya moja kwa moja kwa mkulima

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahshauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Guna Maziku, akizungumza kwenye kikao maalum cha Kamati ya Mazao ya wilayani humo kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU Februari 4,2026, kikilenga kusikiliza changamoto zinazokabili zao la pamba na kuweka mikakati sahihi na ya pamoja katika uboreshaji wa uzalishaji, masoko na manufaa ya moja kwa moja kwa mkulima

Matangazo

  • TANGAZO LA MWALIKO WA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI January 20, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • KISHAPU YAJIPANGA KUONGEZA UZALISHAJI PAMBA

    February 04, 2026
  • BARAZA LA WAFANYAKAZI KISHAPU LAPITISHA MWELEKEO MPYA MASLAHI YA WATUMISHI

    February 03, 2026
  • VIKUNDI 21 MAKUNDI MAALUMU VYAPATIWA MIKOPO KISHAPU

    January 29, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAAZIMIA SOKO HURIA LA PAMBA, LATOA MSISITIZO WA LISHE NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    January 28, 2026
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa