• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
    • Ratiba ya vikao vya kisheria vya MSM
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

KISHAPU YAONGEZA KASI UTEKELEZAJI WA PJT-MMMAM

Posted on: February 19th, 2026

Afisa Ustawi wa Jamii wilayani Kishapu mkoani Shinyanga  Mwajuma Abeid akizungumza wakati akifungua kikao cha utekelezaji wa PJT-MMMAM mwezi Oktoba-Disemba 2025, kwa niaba ya Mganga Mkuu wilayani humo chenye lengo la kupata uelewa wa kadi alama ya tathmini ya maendeleo ya awali ya Mtoto (ECD), Changamoto zilizotambuliwa na njia za kutatua changamoto hizo zinazoikabili programu hiyo Februari 19,2026


Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imeendelea kutekeleza Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT–MMMAM) kwa lengo la kuhakikisha watoto wanapata malezi bora tangu wakiwa katika hatua za awali za maisha.


Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa programu hiyo kwa kipindi cha Oktoba hadi Desemba 2025 Mratibu wa PJT–MMMAM wilayani humo,Paul Lupolaso, Februari 19,2026 kwenye kikoa chenye lengo la kupata uelewa wa kadi alama ya tathmini ya maendeleo ya awali ya Mtoto (ECD), Changamoto zilizotambuliwa na njia za kutatua changamoto hizo na  ambaye ameeleza mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazoikabili programu hiyo.

Mratibu wa PJT–MMMAM wilayani humo,Paul Lupolaso akizungumza kwenye kikao cha utekelezaji wa PJT-MMMAM mwezi Oktoba-Disemba 2025, chenye lengo la kupata uelewa wa kadi alama ya tathmini ya maendeleo ya awali ya Mtoto (ECD), mafanikio yaliyopatikana pamoja na changamoto zinazoikabili programu hiyo na ku Februari 19,2026

Katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka wa fedha 2025/2026, Halmashauri imeendelea kutekeleza shughuli mbalimbali zikiwemo utoaji wa elimu ya afya na lishe kwa jamii, kampeni za kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga, jitihada za kukabiliana na udumavu, pamoja na utoaji wa elimu ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto.

"Katika kipindi hiki tumeweza kutoa vidonge vya madini chuma kwa wanawake wajawzito na kufikia 91%, elimu ya kinamama kujifungulia vituo vya afya 90%, Watoto kunyonya maziwa ya mama pekee wenye umri wa miezi 0 mpaka miezi 6 kwa 98%" ameongeza Lupolaso

Aidha,  ameongeza kuwa elimu ya usalama wa mtoto imeendelea kutolewa katika shule za msingi 128 zilizopo ndani ya Wilaya ya Kishapu. Hata hivyo, amebainisha kuwa utekelezaji wa programu hiyo umekumbana na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa watumishi katika kitengo cha lishe, ushiriki mdogo wa wanaume katika masuala ya afya na lishe ya familia, pamoja na uhitaji wa kuimarisha usimamizi elekezi katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Kutokana na changamoto hizo, Halmashauri imeweka mikakati ya kuimarisha utekelezaji wake kwa kufanya kikao cha Kamati ya Lishe kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata, kuhimiza maadhimisho ya Siku ya Afya na Lishe (SaLiki), kufanya usimamizi elekezi katika vituo vya afya na zahanati, kuongeza uhamasishaji wa jamii kuhusu usafi wa mazingira na umuhimu wa kinamama kujifungulia katika vituo vya afya, pamoja na kutoa mafunzo kazini kwa watoa huduma kuhusu huduma za dharura kwa mama na mtoto.

Baada ya uwasilishaji wa taarifa hiyo, wajumbe walitoa maoni mbalimbali ya kuboresha programu hiyo, wakisisitiza umuhimu wa kuongeza mikakati ya kuwahusisha wanaume katika kliniki za wajawazito na masuala ya lishe ili kuimarisha uwajibikaji wa familia, kuanzisha vikundi vya wazazi katika ngazi ya jamii vitakavyosaidia kutoa elimu ya malezi chanya, pamoja na kuimarisha ukusanyaji wa takwimu sahihi zitakazosaidia katika upangaji na utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya mtoto.


Sambamba na hayo, Halmashauri pia imeendelea kutoa shukrani kwa wadau wanaoiunga mkono katika utekelezaji wa programu hiyo wakiwemo World Vision, THPS, Marie Stopes, AMREF, Kivulini na REDESO kwa mchango wao katika kuboresha ustawi wa watoto na jamii kwa ujumla.


Ikumbukwe kuwa Serikali ilizindua rasmi programu hiyo mwezi Desemba 2021 ikiwa na dhamira ya kuimarisha mfumo jumuishi wa malezi ya mtoto unaojikita katika maeneo ya afya bora, lishe, malezi yenye mwitikio, fursa za ujifunzaji wa awali pamoja na ulinzi na usalama wa mtoto.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA February 16, 2026
  • TANGAZO LA MWALIKO WA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI January 20, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MWENYEKITI KISHAPU ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA AFYA

    February 19, 2026
  • KISHAPU YAONGEZA KASI UTEKELEZAJI WA PJT-MMMAM

    February 19, 2026
  • WAKULIMA WA PAMBA WANAOZINGATIA KANUNI BORA WAPEWA VIFAA VYA PEMBEJEO-KISHAPU

    February 18, 2026
  • KISHAPU YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 54.3 2026/2027

    February 12, 2026
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa