Maafisa Ugani na Wadau wa zao la pamba wametakiwa kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanaongeza uzalishaji na tija kwenye zao la pamba kwa kutoa michango mbalimbali kwasababu wao ni wadau muhimu katika maendeleo ya zao hilo na si wakulima pekee.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi ameyesema hayo leo Machi 11, 2025 wakati wa kikao cha Maafisa Ugani, watendaji wa Vijiji, AMCOS pamoja na Wadau wa Zao la Pamba kilichofanyika katika Ukumbi wa SHIRECU kwaajili ya kutathmini Maendeleo ya Zao la Pamba kwa Wakulima

Akizungumza na Wadau wa Pamba, AMCOS, Bodi ya Pamba, Maafisa Ugani, Watendaji wa Kijiji na Vijana wa BBT amewataka kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha wanakuwa kitu kimoja wanapokutana na changamoto, kero na matatizo katika kipindi hiki ili iwe rahisi katika Kumsaidia Mkulima na kuhakikisha Pamba inapatikana kwa Wingi ili kufikia Malengo yaliyokusudiwa katika uzalishaji wa zao la Pamba

"Mnapotoka hapa mhakikishe mnaenda kukaa pamoja Afisa Ugani, Bodi ya Pamba, Mtu wa BBT, Afisa Ushirika, Mtendaji wa kata mkatafute Solution mnafanyaje ili kufanikisha uzalishaji wa Pamba Mwezi wa Tano, Binadamu ameumbwa kutatua Changamoto za Watu wengine, hamna Binadamu aliyeumbwa kusababisha matatizo ya Watu hivyo mkawe kitu kimoja katika kutatua Changamoto za Wakulima Kwa kushirikia Pamoja" alisema Masindi

Aidha kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mwl Sigthbeth Rwezahula amewataka Maafisa Ugani pamoja na Wadau wa Pamba kushirikiana kwa pamoja ndiyo kuleta Tija katika uzalishaji wa Zao la Pamba 2025 na Miaka ijayo
Aidha DC Masindi amepiga Marufuku Maafisa Ugani kujihusisha na Shughuli zingine tofauti na Kilimo, Shughuli ambazo zinapelekea kushindwa kuwahudumia Wakulima wa Zao la Pamba ipasavyo
Pia amewataka wataalamu wa kilimo Wilayani Kishapu kuendelea kutoa Elimu kwa wakulima wa zao la pamba kuzingatia taratibu za kilimo cha zao hilo ili kuongeza tija na uzalishaji na kuacha kilimo cha mazoea.
Hata na Hivyo Wakulima Wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt, Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali katika kilimo cha Pamba licha ya Changamoto ndogondogo kama vile Sumu kwaajili ya kupulizia wadudu kutokufika kwa Wakati.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa