• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

MBUNGE BUTONDO ATOA VIFAA VYA TEHAMA KUUNGA MKONO SEKTA YA ELIMU KISHAPU

Posted on: May 26th, 2025

Mbunge wa Jimbo la Kishapu, Mheshimiwa Boniphace Butondo, ameendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuboresha sekta ya elimu nchini kwa kukabidhi vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika shule za sekondari Ngofila na Lagana.

Zoezi hilo limefanyika jana katika shule hizo kwa nyakati tofauti, ambapo Mbunge Butondo aliambatana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kishapu, Shija Ntelezu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mheshimiwa Butondo alisema lengo la msaada huo ni kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuinua kiwango cha elimu kwa kuwezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo na kuongeza ufaulu.

“Vifaa vya TEHAMA nilivyokabidhi ni pamoja na printer, seti kamili ya monitá, CPU na projector. Vifaa hivi vitasaidia kuinua taaluma ya wanafunzi na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia,” alisema Butondo.

Aliongeza kuwa vifaa hivyo vitarahisisha kazi kwa walimu katika maandalizi ya masomo na uchapaji wa mitihani, hivyo kuondoa utegemezi kwa vituo binafsi vya uchapaji na kupunguza gharama za uendeshaji.

Mbunge huyo pia alitoa maelekezo kuwa vifaa hivyo vitunzwe kwa umakini, mazingira ya matumizi yawe safi, na kusisitiza uanzishwaji wa somo la Kompyuta katika shule ya sekondari Lagana ambayo kwa sasa haina somo hilo.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Ngofila, Bi. Matrida Mwaliaje, alieleza kuwa upatikanaji wa vifaa hivyo ni chachu ya kuongeza ufaulu, kwani sasa wanafunzi watakuwa wanapatiwa majaribio mara kwa mara ili kutathmini maendeleo yao ya kitaaluma.

Amesema vifaa hivyo pia vitapunguza gharama na adha ya kusafiri umbali mrefu hadi shule za Kishapu na Ukenyenge, zilizoko zaidi ya kilomita 60, kwa ajili ya kuchapisha mitihani.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Lagana, Bw. Adam Malongo, alishukuru kwa msaada huo akisema ni mchango mkubwa katika kuinua viwango vya elimu shuleni hapo.

Baadhi ya wanafunzi, wakiwemo Hadija Pambe, walionesha furaha yao kwa kupatiwa vifaa hivyo, wakisema vitawawezesha kusoma kwa vitendo na kufanya majaribio ya mitihani mara kwa mara.

Naye Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kishapu, Bw. Shija Ntelezu, alitoa pongezi kwa Mbunge Butondo kwa kuendelea kutekeleza kwa vitendo Ilani ya Chama Cha Mapinduzi, hasa katika sekta ya elimu.

Hadi sasa, Mbunge Butondo ameshakabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule tatu za sekondari jimboni humo, ambazo ni Kishapu, Ngofila na Lagana.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • RC MHITA AFANYA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI NA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI KISHAPU.

    January 10, 2026
  • RC MHITA AWATAKA MADIWANI KISHAPU KUDUMISHA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO - NGUZO KUFANIKISHA MIPANGO YA MAENDELEO.

    December 19, 2025
  • DED JOHNSON ATOA MAELEKEZO MUHIMU KWA MADEREVA

    December 19, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WAMTEUA MWENYEKITI MPYA HALMASHAURI YA WILAYA KISHAPU

    December 03, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa