Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Joseph Swalala akiwasikiliza wajumbe wa kikao hicho wakati wakijadili mwenendo wa kampeni za Uchaguzi kwa Vyama vya siasa Septemba 29,2025 Katika Ukumbi wa Halmashauri hiyo
Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Joseph Swalala amekutana na Kamati ya Ulinzi na usalama, Viongozi wa dini,Viongozi wa vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi Kwa ajili ya kupata mrejesho wa mwenendo wa Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.
Kikao hicho kimefanyika Septemba 29,2025 katika Ukumbi wa Halmashauri ambapo pia wajumbe hao wamepewa maelekezo ya upigaji kura ya Rais kupitia mfumo wa kujaza fomu (KRP) Kwa Wananchi waliojiandikisha nje ya Jimbo hilo pamoja na wajumbe kupewa maelekezo ya kuandaa majina ya mawakala wa vyama vya siasa.










Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa