• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

REDESO NA CARE INTERNATIONAL WAWEZESHA WAKULIMA WADOGO KISHAPU KUPITIA MRADI WA UFUGAJI WA KUKU NA ZAO LA MKONGE

Posted on: May 30th, 2025

Katika kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, Shirika lisilo la kiserikali la Relief to Development Society (REDESO) kwa kushirikiana na CARE International, limeendelea kuwawezesha wakulima wadogo wilayani Kishapu kwa kuwajengea uwezo katika mnyororo wa thamani wa kilimo cha mkonge na ufugaji wa kuku wa kisasa.

Akizungumza wakati wa ziara ya mafunzo kwa wakulima katika vijiji vya Isoso na Negezi Mei 29,2025 Meneja Miradi kutoka REDESO, Bw. Charles Bulegeya alisema kuwa mradi huo unalenga kuwawezesha wakulima na wafugaji wadogo kwa kuwapatia elimu ya vitendo na mitaji midogo ya kuanzisha shughuli za uzalishaji zenye tija.

Meneja miradi Redeso Kishapu Charles Buregeya(kushoto),afisa wa Redeso Kishapu Erica Karuta (katikati) na afisa mradi Care International Wilfred Makombe(kulia) 

“Tunatoa mafunzo ya mbinu bora za ufugaji wa kuku chotara walioboreshwa, wenye uwezo wa kustahimili magonjwa, kukua haraka na kuongeza kipato. Lengo ni kuwajengea uwezo ili nao wawe wawezeshaji katika jamii zao,” amesema Bulegeya.

Afisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Kalekwa Mtoni na mwezeshaji katika semina iliyoandaliwa na Redeso Kishapu kwa kushirikiana na Care International katika ukumbi wa Veta Wilayani humo Mei 29,2025

Mafunzo hayo yamehusisha pia ziara za mafunzo kwa wakulima kutembelea miradi iliyofanikiwa ili kujifunza kwa vitendo, kubadilishana uzoefu, na kupata motisha kutoka kwa wenzao waliofanikiwa katika ufugaji wa kuku na kilimo cha mkonge.

Afisa Mifugo wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Bw. Kalekwa Mtoni ambaye pia ni mmoja wa wawezeshaji wa mafunzo hayo, amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa kushirikiana na Halmashauri ili kufikia lengo la Mkurugenzi wa Halmashauri, Bw. Emmanuel Johnson, la kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi huku wakiboresha lishe katika familia zao.

“Tumepewa elimu ya bure yenye thamani kubwa, ni jukumu letu kuitumia vizuri kwa ajili ya maendeleo ya familia zetu na jamii kwa ujumla,” amesema Mtoni.

 Diwani wa Viti Maalum Kata ya Ukenyenge, Mhe. Josephine Malima, amewapongeza REDESO na CARE International kwa juhudi zao za kuwawezesha wananchi kupitia elimu ya kilimo na ufugaji wa kisasa.

Meneja Mradi kutoka CARE International, Bw. Wilfred Makombe, amehimiza wanakikundi na wawezeshaji kutumia rasilimali zilizopo kuanzisha miradi badala ya kusubiri mazingira bora yasiyopatikana kwa urahisi.

“Tumeshuhudia mafanikio ya wanakikundi kutoka Negezi na Busongo waliotumia vifaa vya kawaida kama bikobiko, lakini sasa wananufaika. Hatupaswi kusubiri miundombinu ya kisasa ili kuanza,” amesema Makombe.

Baadhi ya wanufaika wa mafunzo hayo, wakiwemo Suzan Ezekiel (Busongo), Rahel Charles (Mihama), Reuben Nestory, Fredina Said (Negezi), na Lata Pungu (Kakola), wameeleza mafanikio yao baada ya kushiriki katika mradi huo.

“Tuliona ufugaji wa kuku ni jambo la kawaida, lakini sasa tunapata kipato cha kusomesha watoto wetu na kuboresha lishe. Kuku ni mfalme!” amesema Suzan Ezekiel, Katibu wa Kikundi cha Muungano, Busongo.

Mradi huu wa miaka mitatu ulioanza mwaka 2023, unatekelezwa na REDESO kwa ushirikiano na CARE International katika vijiji 10 vya Wilaya ya Kishapu ambavyo ni Shagihilu, Mihama, Busongo, Negezi, Uchunga, Kakola, Lubaga, Bubinza, Isoso na Unyanyembe. Mpaka sasa mradi umefikia asilimia 98 ya utekelezaji, na kwa sasa zaidi ya vifaranga 2000 vya kuku chotara huagizwa kila mwezi.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • DC MASINDI ATAKA WAUGUZI KISHAPU WAFANYE KAZI KWA NIDHAMU NA UPENDO

    May 31, 2025
  • REDESO NA CARE INTERNATIONAL WAWEZESHA WAKULIMA WADOGO KISHAPU KUPITIA MRADI WA UFUGAJI WA KUKU NA ZAO LA MKONGE

    May 30, 2025
  • MBUNGE BUTONDO ATOA VIFAA VYA TEHAMA KUUNGA MKONO SEKTA YA ELIMU KISHAPU

    May 26, 2025
  • CPA. MAKALA AIPONGEZA SERIKALI MAENDELEO KISHAPU – BUTONDO AOMBA DED ASIONDOLEWE

    May 23, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa