• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

REO HAULE AZINDUA MFUMO WA UJIFUNZAJI WA UMAHIRI KWA NJIA YA SAUTI KISHAPU

Posted on: October 1st, 2025

Afisa Elimu wa Mkoani Shinyanga Samson Hango Halute ambaye pia ni mgeni rasmi akizungumza kwenye uzinduzi wa mfumo wa Ujifunzaji wa Umahiri kwa Njia ya Sauti (AICBL) Shule ya Sekondari ya Wavulana Shinyanga iliyoko Wilayani Kishapu Septemba 30,2025

Afisa Elimu wa Mkoa wa Shinyanga, ambaye pia ni mgeni rasmi katika uzinduzi wa Ujifunzaji wa Umahiri kwa Njia ya Sauti (AICBL) Samson Hango Halute amesema kuwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kuhitaji walimu wabunifu wanaoweza kuibua mbinu na zana za ufundishaji zinazowasaidia wanafunzi kuelewa kwa urahisi kwani ubunifu wa walimu ni nyenzo muhimu katika kuboresha matokeo ya kielimu na kuongeza umahiri wa wanafunzi Shuleni.

Katika hotuba yake wakati wa uzinduzi wa mfumo huo Septemba 30,2025 Shule ya Sekondari Shinyanga Afisa Elimu huyo ametoa pongezi kwa Mwalimu David Ipamba, Mratibu na Mbunifu wa maabara ya Jiografia katika Shule ya Sekondari Shinyanga, pamoja na wanafunzi waliohusika katika ubunifu huo. Ameleza kuwa huo ni ushahidi wa ushirikiano chanya kati ya Walimu na Wanafunzi katika kukuza ubunifu wa kitaaluma. Aidha, amenukuu methali ya kielimu isemayo: “Mafunzo ya nadharia yana tabia ya kusahaulika, lakini ukiona utaelewa, ukitenda utakumbuka na utaelewa, na ukielewa hutasahau.”


Afisa huyo amesisitiza kuwa kutokana na ubunifu huo, Shule ya Sekondari Shinyanga inapaswa kuwa mfano wa kuigwa katika Mkoa mzima, na ametoa wito Kwa Walimu na Wanafunzi kuhakikisha kuwa mwanafunzi wa kwanza kitaifa kwa somo la Jiografia anatokea shuleni hapo.

Afisa Elimu wa Mkoani Shinyanga Samson Hango akizindua mfumo wa Ujifunzaji wa Umahiri kwa Njia ya Sauti (AICBL) Shule ya Sekondari ya Wavulana Shinyanga iliyoko Wilayani Kishapu Septemba 30,2025

Sambamba na hayo amewataka Wanafunzi kuendelea kuongeza bidii zaidi kwenye masomo yao wakiendelea kubuni vitu mbalimbali huku waalimu wa Shule zisizokuwa na maabara ya somo hilo kujifunza kupitia Shinyanga Sekondari iliyoko Wilayani Kishapu.

Amempongeza kuwa Mwl.David Ipamba ambaye ni Mratibu na Mbunifu wa maabala ya Jiografia shuleni hapo na Wanafunzi wote waliohusika kwenye ubunifu huo akisesema hatua hiyo itathibitisha kuwa ubunifu wa vifaa vya kufundishia unaleta matokeo chanya kwa maendeleo ya elimu nchini.

"Mafunzo ya nadharia yanatabia ya ukisikia utasahau,ukiona utakumbuka,ukitenda utakumbuka na utaelewa na pia ukielewa hautasahahu hivyo natamani kuona mwanafunzi wa kwanza Kitaifa wa somo la Jiografia anatokea shulen hapa" ameongeza Halute

Afisa Elimu Sekondari Wilayani Kishapu Moshi Balele Moshi akizungumza kwenye uzinduzi wa mfumo wa Ujifunzaji wa Umahiri kwa Njia ya Sauti (AICBL) Shule ya Sekondari ya Wavulana Shinyanga iliyoko Wilayani Kishapu Septemba 30,2025
Hata hivyo Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Wilayani Kishapu Moshi Balele Moshi amepongeza jitihada hizo zilizofanyika ndani ya Wilaya hiyo huku akihimiza uboreshaji zaidi wa zana za ujifunzaji na kufundishia

Mratibu na Mbunifu wa mpango wa Ujifunzaji wa Umahiri Kwa Njia ya (AICBL) Mwl.David P. Ipamba amesema mpango huo wa ujifunzaji umebuniwa ili kuendeleza mbinu shirikishi za kujifunza zinazowahusisha Wanafunzi katika kusikiliza, kufanya na kushirikiana. Kupitia matumizi ya sauti, modeli na mbinu za vitendo, wanafunzi huchochewa kufikiri kwa kina, kuendeleza ubunifu na kujenga uelewa mpana wa masuala mbalimbali.

Mwl. Ipamba amesema njia hiyo itawawezesha sio tu kuwa wasikilizaji pekee, bali washiriki wa moja kwa moja katika mchakato wa kupata maarifa.AICBL pia inalenga kuwatengeneza wanafunzi wenye stadi za karne ya 21 kwa kuwafundisha namna ya kufikiri kwa ubunifu, kushirikiana na kujenga ujuzi wa mawasiliano huku ikigusa matumizi ya TEHAMA.

"Mfumo huu huondoa dhana ya kujifunza kwa kukariri pekee na badala yake unaimarisha uwezo wa mwanafunzi kutafsiri nadharia kwa vitendo kupitia maabara na mazingira halisi ya kila siku. Kupitia njia hii, elimu inakuwa na tija kwa maisha ya sasa na yajayo"ameongeza Ipamb.

Dhamira kubwa ya AICBL ni kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi, wakiwemo wenye uhitaji maalumu, anafikiwa kwa kutumia sauti, picha au mguso. Mfumo huu unajikita katika kujenga msingi wa uelewa endelevu unaoweza kuendelezwa hata nje ya darasa kupitia redio, simu au tablet. Kwa njia hii hivyo AICBL inaleta mageuzi ya elimu yanayolenga kukuza vizazi vya wabunifu, wachambuzi na viongozi wa kesho

Mratibu na Mbunifu wa mpango wa Ujifunzaji wa Umahiri Kwa Njia ya (AICBL) Mwl.David P. Ipamba akizungumza kwenye uzinduzi wa mfumo wa Ujifunzaji wa Umahiri kwa Njia ya Sauti (AICBL) Shule ya Sekondari ya Wavulana Shinyanga iliyoko Wilayani Kishapu Septemba 30,2025

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Sekondari Shinyanga Benard Ishengoma inaendelea kuweka mikakati madhubuti ya kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia ili kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora na yenye tija kwa maisha yao ya sasa na ya baadaye.

"Tumejipanga kuongeza ubunifu katika matumizi ya TEHAMA, kusimamia nidhamu ya wanafunzi kwa ukaribu zaidi, na kuhakikisha kila mwanafunzi anapata nafasi ya kushiriki kikamilifu katika masomo na shughuli za ziada zinazojenga ujuzi na weledi" amesema Ishengoma

Amesema wanatambua mchango mkubwa wa Serikali, wadau wa elimu, pamoja na wazazi na walezi katika kufanikisha safari ya kitaaluma ya wanafunzi hivyo watajitahidi kuendeleza mshikamano huo kwa kushirikiana bega kwa bega katika kushughulikia changamoto zilizopo, huku wakilenga kuongeza ufaulu, nidhamu, na ubunifu wa wanafunzi.
Mkuu wa Shule Wavulana ya Shinyanga Sekondari Wilayani Kishapu Mkaoni Shinyanga Mwl Bernard Ishengoma akizungumza kwenye uzinduzi wa mfumo wa Ujifunzaji wa Umahiri kwa Njia ya Sauti (AICBL) Shule ya Sekondari ya Wavulana Shinyanga iliyoko Wilayani Kishapu Septemba 30,2025

"Kwa pamoja, tunaamini Shule ya Sekondari Shinyanga itaendelea kuwa chachu ya mafanikio na kielelezo cha ubora wa elimu katika Mkoa wa Shinyanga na Taifa kwa ujumla" ameongeza.

Shule ya Sekondari Shinyanga iliyoko Kijiji Cha Wizunza Kata ya Mwadui Lohumbo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ilianzishwa mwaka 1966 na sasa ikiwa ni Shule Jumuishi ikiwa na jumla ya Wanafunzi 930 kuanzia kidato Cha kwanza hadi kidato Cha sita ambapo Wanafunzi wenye mahitaji maalum wakiwa ni 118.


Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

    November 21, 2025
  • WATUMISHI KISHAPU WAPEWA MAFUNZO YA ELIMU YA FEDHA NA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

    November 20, 2025
  • DC,DED NA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI JIMBO LA KISHAPU WAUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA

    October 29, 2025
  • WASIMAMIZI WA VITUO KISHAPU WAONYWA KUTOKUWA CHANZO CHA MIGOGORO

    October 27, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa