Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga Bw.Joseph Swalala
Vyama vinne vya siasa vimepeleka wagombea wake kuchukua fomu za kugombea Ubunge katika Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo Bw. Joseph Swalala.
![]()
Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama Makini Bi.Perpetua Kabete(kushoto) akipokea fomu ya uteuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Bw.Joseph Swalala(kulia) Agosti 14,2025
Wagombea hao wamechukua fomu pamoja na miongozo ya uchaguzi kwa ajili ya kupata uelewa wa namna wanavyopaswa kuenenda katika kipindi cha kampeni hadi Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Vyama vilivyothibitisha ushiriki wake mpaka leo Agosti 22 ni Chama Cha Makini, Sauti ya Umma (SAU), Democratic Party (DP) na National Reconstruction Alliance (NRA).
Zoezi la uchukuaji fomu linatarajiwa kuhitimishwa ifikapo Agosti 27, 2025

Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga kupitia Chama Cha Sauti ya Umma(SAU) Bi.Siwema John Silas Agosti 15,2025

Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama cha Democratic Party (DP) Bi. Vida Wilson Rubete(kushoto) akipokea fomu ya uteuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Bw.Joseph Swalala(kulia) Agosti 18,2025

Mgombea Ubunge Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga kwa tiketi ya Chama Cha National Reconstruction Alliance (NRA) Bw.Edward Blandit Jisandu akiwa ameshikilia fomu na miongozo mbalimbali ya Uchaguzi baada ya kupokea kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Bw.Joseph Swalala Agosti 22,2025
Picha ya pamoja ya viongozi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jimbo la Kishapu na mgombea Ubunge Jimbo hilo kwa Tiketi ya Chama Makini

Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa