• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
    • Ratiba ya vikao vya kisheria vya MSM
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

WAKULIMA WA PAMBA WANAOZINGATIA KANUNI BORA WAPEWA VIFAA VYA PEMBEJEO-KISHAPU

Posted on: February 18th, 2026

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, akizungumza na baadhi ya wakulima wa zao la pamba Kata ya Mwamashele wilayani humo kwenye ziara yake  kwenye Kata hiyo na Kata ya Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, Februari 18, 2026 ametembelea Kata za Mwamashele na Lagana kwa lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo.

Mkaguzi wa zao la  Pamba wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kutokea Bodi ya pamba mkoani Mwanza Joachimu John Gabanya, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026

Katika ziara hiyo iliyojaa hamasa na matumaini mengi kwa wakulima, Mhe. Masindi amesisitiza umuhimu wa kuzingatia kanuni za kilimo bora ikiwemo upandaji kwa mistari, matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na ufuatiliaji wa karibu wa mashamba ili kuongeza tija na mavuno yenye ubora.

Akiwahimiza wakulima kuongeza uzalishaji, amesema Serikali imejipanga kikamilifu kuhakikisha mkulima wa pamba anainuliwa kiuchumi kupitia uwezeshaji wa pembejeo na usimamizi wa kitaalamu wa kilimo.


“Watumieni vijana wa BBT ili kuwa na kilimo chenye tija na chenye matokeo chanya. Ushirikishwaji wao utaongeza nguvu kazi na maarifa mashambani,” amesisitiza Mhe. Masindi.

Diwani wa Kata ya Mwamashele wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Lucas Daudi Nkende, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026

Ameongeza kuwa ugawaji wa vifaa vya pembejeo unalenga kuwafikia wakulima wanaozingatia kanuni za kilimo bora, ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha uwekezaji wa Serikali unazaa matokeo yenye manufaa kwa mkulima mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.


Kwa upande wake, Mkaguzi wa zao la  Pamba wilayani humo, Joachimu John Gabanya  akizungumza wakati wa ziara hiyo, amewataka wakulima kutunza vifaa walivyopokea na kuvitumia kwa uangalifu ili viendelee kuwasaidia kwa muda mrefu na kuongeza ufanisi katika uzalishaji.

Miongoni mwa wakulima walionufaika na ziara hiyo ni Juma Paul Njile, mkulima mwenye ekari 37 kutoka Kata ya Mwamashele, ambaye ameeleza mafanikio aliyoyapata kupitia kilimo cha pamba kinachofuata misingi sahihi ya kitaalamu.

“Miaka ya nyuma nilifanya majaribio ili kubaini kama tunachoambiwa na wataalamu ni sahihi kuhusu ubovu wa mazao mseto, hivyo niliamua kulima shamba mseto moja na lingine sikulichanganyia zao jingine bali pamba peke yake kwenye lile shamba mseto nilipata mavuno machache, lakini lile nililolima kwa kufuata kanuni za kilimo bora, niliona faida kubwa. Kilimo hiki kinalipa. Msimu huu wa 2026/2027 natarajia kuvuna kilo 3,700,” amesema kwa kujiamini.

Mratibu wa zao la  Pamba Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Richard Manguha, akizungumza kwenye ziara ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kata ya Mwamashele na Lagana yenye lengo la kufuatilia kwa karibu maendeleo ya zao la pamba, hali ya nyenzo za upuliziaji sumu pamoja na ugawaji wa vifaa vya pembejeo kwa wakulima waliokidhi vigezo Februari 18,2026

Sambamba na hilo, Mkuu wa Wilaya ameshuhudia matumizi ya nyenzo za upuliziaji sumu katika baadhi ya mashamba na kugawa jumla ya vifaa vya pembejeo aina ya Solo pump 19 kwa wakulima waliokidhi vigezo katika Kijiji cha Mihama, Kata ya Lagana ikiwa ni miongoni mwa solo pump 1000 zilizopokelewa Wilayani humo.


Ziara hiyo imeacha alama ya matumaini, ikionyesha dhamira ya Serikali ya kuimarisha zao la pamba kama mhimili muhimu wa uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI YA MKATABA February 16, 2026
  • TANGAZO LA MWALIKO WA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI January 20, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MWENYEKITI KISHAPU ARIDHISHWA NA HUDUMA ZA AFYA

    February 19, 2026
  • KISHAPU YAONGEZA KASI UTEKELEZAJI WA PJT-MMMAM

    February 19, 2026
  • WAKULIMA WA PAMBA WANAOZINGATIA KANUNI BORA WAPEWA VIFAA VYA PEMBEJEO-KISHAPU

    February 18, 2026
  • KISHAPU YAPITISHA BAJETI YA BILIONI 54.3 2026/2027

    February 12, 2026
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa