• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Nyaraka
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • Matangazo
    • Sheria ndogo ya ushuru wa huduma
    • Mifumo
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Biashara
    • ujasiliamali
    • Kilimo
    • Uvuvi
      • Uvuvi wa Samaki katika Bwawa la Songwa, Bwawa mhumbu
    • Ufugaji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
      • Mhe. William Luhende Jijimya - Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Francis Manyanda - Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Mhe. Joel Ndettoson - Diwani kata ya Kishapu
      • Mhe. Mohamed Aman - Diwani kata ya Ndoleleji
      • Mhe. Lucas Nkende - Diwani kata ya Mwamashele
      • Mhe. Pontias Daud - Diwani kata ya Mwataga
      • Mhe. James Kasomi - Diwani kata ya Bubiki
      • Mhe. Bushi Mpina - Diwani kata ya Mwamalasa
      • Mhe. Nyama Kisinza - Diwani kata ya Somagedi
      • Mhe. Mashini W. Washima - Diwani kata ya Uchunga
      • Mhe. Anderson Mandia - Diwani kata ya Ukenyenge
      • Mhe. Edward Manyama - Diwani kata ya Kiloleli
      • Mhe. Reuben Siyabo - Diwani kata ya Bupigi
      • Mhe. Bujiku Nyanda - Diwani kata ya Mwaweja
      • Mhe. Michael Paul - Diwani kata ya Shagihilu
      • Mhe. Luhende S. Luhende - Diwani kata ya Lagana
      • Mhe. Richard Dominico - Diwani kata ya Talaga
      • Mhe. James Kamuga - Diwani kata ya Igaga
      • Mhe. Lameck Nsubata - Diwani kata ya Itilima
      • Mhe. Mpemba Malangahe - Diwani kata ya Bunambiyu
      • Mhe. Makenzi Charles - Diwani kata ya Busangwa
      • Mhe. Nestory Kalugula - Diwani kata ya Ngofila
      • Mhe. Lwinzi Kidiga - Diwani kata ya Maganzo
      • Mhe. Samson Gelewa - Diwani kata ya Mwasubi
      • Mhe. Sarah Marco - Diwani kata ya Idukilo
      • Mhe. Enock Bundala - Diwani kata ya Masanga
      • Mhe. Thabidha Mmbando - Diwani kata ya Mwakipoya
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya Mwenyekiti wa Halmashauri
  • miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayotekelezwa
    • Miradi iliyokamilika
  • Kituo Cha Habari
    • maktaba ya picha
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Taarifa za Vyombo vya Habari
  • Maeneo
    • Kata
      • Orodha ya Kata
    • Tarafa
      • Orodha ya Tarafa
    • Vijiji
      • Orodha ya Vijiji

WANANCHI 1,200 VIJIJI VYA MFANO KISHAPU WAPEWA HATI MILKI ZA KIMILA

Posted on: July 23rd, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe.Peter Masindi akikabidhi hati milki ya kimila kwa wananchi wa Kijiji cha mfano cha Mwadui Lohumbo Kata ya Mwadui Lohumbo Wilayani humo Julai 23,2025 wakiwa ni miongoni mwanufaika wa Vijiji 16 vinavyozunguka migodi ya Williamson na Al hilali kwenye mpango wa Tume ya taifa ya mpango wa Matumizi ya ardhi

Wananchi 1,200 kutoka Vijiji vya Mwaduhi Lohumbo na Idukilo, Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga, wamekabidhiwa hati za kimila zinazowapa haki halali ya umiliki wa ardhi, hatua inayotarajiwa kuboresha maisha yao kijamii na kiuchumi.

Zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa matumizi bora ya ardhi unaosimamiwa na Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, ambapo vijiji 16 vinavyozunguka mgodi wa Williamson na Al hilal na kutengwa vijiji viwili vya mfano ikiwa ni pamoja na Idukilo na Mwaduhi Lohumbo.

Hati hizo zimekabidhiwa kwa wananchi Julai 23, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi ambaye amesisitiza umuhimu wa hati hizo na matumizi yake sahihi kwa maendeleo ya wananchi.

Akizungumza na wananchi wakati wa makabidhiano hayo, Mhe. Masindi amesema kuwa hati hizo zimetolewa bure chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, hivyo wananchi wanapaswa kuzihifadhi vizuri na kuzingatia thamani yake.

"Serikali ya Mhe. Samia imewapa hati ambazo hamjazigharamikia chochote. Huu ni urithi wa thamani. Mtu asiye na umiliki wa ardhi anadharaulika; ardhi yenye thamani ni ile inayotambulika kisheria,” amesema Mhe. Masindi.

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi 

Amehimiza pia matumizi ya hati hizo kama dhamana za kupata mikopo kwenye taasisi za kifedha, jambo ambalo linaweza kuibua fursa za biashara, kilimo cha kisasa na kuimarisha uchumi wa familia na jamii

Akihimiza kasi ya utekelezaji wa mpango huo, Mhe. Masindi amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kishapu Emmanuel Johnson kuhakikisha Vijiji vilivyobakia kati ya 16 vinaingizwa kwenye mpango wa matumizi bora ya ardhi.

Kwa upande wake, Mratibu wa zoezi hilo kutoka Tume ya Matumizi ya Ardhi Edward Mpanda amesema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa huku wengi wakionesha hamasa ya kutaka mpango huo kuendelezwa zaidi.

Mratibu wa mradi kutoka Tume ya taifa ya mpango wa matumizi ya ardhi Edward Mpanda akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Mhe Peter Masindi alipokuwa akikabidhi hati za kimila kwa wananchi wa Vijiji viwili vya mfano Mwadui Lohumbo na Idukilo kati ya Vijiji 16 vilivyokuwa kwenye mradi wa mpango wa matumizi ya ardhi Julai 23,2025

“Mwanzoni kulikuwa na changamoto ya mwamko, lakini baada ya elimu kutolewa na wananchi kuelewa faida zake, tumeshuhudia ushiriki mkubwa,tunaishukuru Serikali na uongozi wa Wilaya kwa kuipa kipaumbele haki ya ardhi kwa kila mwananchi,” amesema Mpanda.

Nae Mkurugenzi wa Halmashauri Bw.Emmanuel Johnson ametoa wito kwa wananchi kutambua thamani ya mipango waliyoiweka katika matumizi ya ardhi, akisisitiza umuhimu wa kutovamia maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma.

“Wananchi mheshimu mipango yenu msivamie maeneo ya huduma kama shule, zahanati au Barabara hata makaburi na masoko,badala yake tumieni muda wenu mwingi kufanya shughuli za maendeleo na kiuchumi,” amesema Johnson.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga BW. Emmanuel Johnson akizungumza wakati Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe Peter Masindi alipokuwa akikabidhi hati za kimila kwa wananchi wa Vijiji viwili vya mfano Mwadui Lohumbo na Idukilo kati ya Vijiji 16 vilivyokuwa kwenye mradi wa mpango wa matumizi ya ardhi Julai 23,2025

Baadhi ya wananchi walionufaika na hati hizo wamesema hatua hiyo ni ukombozi mkubwa huku Anna Elikana kutoka Kijiji cha Idukilo amesema kuwa hati hiyo italinda familia yake dhidi ya migogoro ya ardhi, hasa kati ya wake kwa waume.

“Wanaume wamekuwa wakiuza viwanja bila kuwashirikisha wake zao sasa tuna nyaraka halali, tuko salama,” amesema Anna kwa furaha.

Zabron Kulwa kutoka Kijiji cha Mwadui Lohumbo ameongeza kuwa mpango huu umekuwa mkombozi wa wanawake na watoto, ambao mara nyingi wamekuwa waathirika wa migogoro ya ardhi na unyanyasaji wa mali huku wakijikwamua kiuchumu kwa kupata elimu ya mikopo.

Hatua ya serikali kutoa hati 1,200 za kimila Wilayani Kishapu si tu ishara ya dhamira ya serikali katika kulinda haki za ardhi kwa wananchi na kuondoa migogoro ya ardhi, bali pia ni kichocheo cha maendeleo ya kiuchumi, kijamii na kijinsia.

Mpango huu unatoa dira ya matumaini kwa maelfu ya wananchi wanaotegemea ardhi kama msingi wa maisha yao ikiwa na maana kuwa maendeleo ya kweli yanaanzia na umiliki halali wa rasilimali.

Matangazo

  • TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA KWA KIPINDI KILICHOISHIA TAREHE 30 JUNE. 2022 August 14, 2023
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI November 03, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MCHAKATO WAANZA UJENZI DAMPO LA KISASA KISHAPU KUIMARISHA USAFI WA MAZINGIRA

    July 26, 2025
  • RC MHITA AFANYA ZIARA YA KIKAZI KISHAPU

    July 22, 2025
  • WANANCHI 1,200 VIJIJI VYA MFANO KISHAPU WAPEWA HATI MILKI ZA KIMILA

    July 23, 2025
  • LISHE BORA YAPAA SHULENI KISHAPU

    July 16, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa