• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Huduma za Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
      • Fedha na Uhasibu
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
    • Ratiba ya vikao vya kisheria vya MSM
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Mpango Mkakati
    • Sheria ndogo ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

WASIMAMIZI WASAIDIZI WA UCHAGUZI KISHAPU WAJENGEWA UWEZO

Posted on: August 4th, 2025

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Mkoani Shinyanga, Bw. Joseph Sahani Swalala akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya Kata Agosti 4,2025 katika Ukumbi wa Mwadui

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga, Bw. Joseph Sahani Swalala, amewataka wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kuhakikisha wanasimamia mchakato wa uchaguzi kwa weledi, uadilifu na umakini mkubwa, ili kuepuka vurugu na malalamiko katika kipindi chote cha uchaguzi.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao leo Agosti 4, 2025, katika Ukumbi wa Mwadui Wilayani humo Bw. Swalala amesema wajibu waliopewa ni mkubwa, hivyo unahitaji nidhamu ya hali ya juu na uwajibikaji wa kweli.

"Mmeaminiwa kusimamia zoezi nyeti kwa Taifa, hivyo zingatieni maadili ya kazi hii, fuateni taratibu, msijihusishe na upendeleo wa aina yoyote, na hakikisheni mnatimiza majukumu yenu kwa haki hadi mwisho wa uchaguzi," amesisitiza Swalala.

Amewataka kutumia mafunzo hayo kama fursa ya kujiongezea maarifa na kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa chaguzi, ili kuhakikisha kuwa kila hatua ya mchakato inatekelezwa kwa ufanisi bila kuibua migogoro au uvunjifu wa amani.

Katika hatua nyingine, Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. Johanita Projest, amewaapisha wasimamizi hao kwa kiapo maalum cha kutoshiriki au kujiusisha na shughuli yoyote ya kisiasa katika kipindi chote cha uchaguzi.

Mhe. Johanita amewakumbusha kuwa nafasi waliyopewa ni ya kisheria na hivyo wanapaswa kuwa waadilifu, waaminifu, na kutunza siri za kazi wanazozifanya kwa mujibu wa sheria za uchaguzi.

“Kiapo mlichokula ni agano mbele ya sheria na mbele ya jamii. Msikubali kutumika kwa namna yoyote ambayo inaweza kuvuruga uchaguzi au kuvunja amani katika Kata zenu,” ameeleza.

Mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu wa kuchagua Rais,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Octoba Mwaka huu, ambapo wasimamizi wasaidizi wa kata ndio kiungo muhimu katika kuhakikisha kila hatua ya mchakato wa uchaguzi inatekelezwa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC).

Matangazo

  • TANGAZO LA MWALIKO WA MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI January 20, 2026
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI December 22, 2025
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • VIKUNDI 21 MAKUNDI MAALUMU VYAPATIWA MIKOPO KISHAPU

    January 29, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAAZIMIA SOKO HURIA LA PAMBA, LATOA MSISITIZO WA LISHE NA BIMA YA AFYA KWA WOTE

    January 28, 2026
  • DED KISHAPU AKABIDHI VIFAA VYA TEHAMA KUWAWEZESHA WAALIMU WENYE CHANGAMOTO YA UONI

    January 28, 2026
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPOKEA NA KUJADILI TAARIFA ZA KATA ROBO YA PILI 2025/2026

    January 27, 2026
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa