Baraza la Madiwani katika wilaya ya Kishapu wamefanya kikao kujadili taarifa za kata Robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichoketi kwa siku mbili kuanzia tarehe 19/05/2020 hadi tarehe 20/05/2020 katika ukumbi wa Soko la Wajasiriamali wilayani Kishapu. Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mheshimiwa Boniphace Butondo ambaye ni Diwani wa kata ya Lagana.
Katika kikao hicho kila Mjumbe aliwasilisha tarifa za kata yake ambapo katika wilaya ya Kishapu kuna jumla ya kata 29 na madiwani 33.
Aidha wajumbe walijadili hali ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na kirusi aina ya Corona katika Wilaya ya Kishapu. Ambapo wawaalamu wa Afya walisema hali ni nzuri kwani hadi sasa hakuna mgonjwa wa corona katika wilaya ya Kishapu hivyo watu wazidi kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa Afya ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka.
Katika kikao hicho Mwenykiti wa Halmashauri alisisitiza halmashauri kupitia wataalamu wake wakusanye mapato kwa wingi kupitia vyanzo mbalimbali kama vile shendi za mabasi, mifugo, mazao maduka n.k
“tutengeneze mikakati ya pamoja na sote tutoke kwa ajili ya kwenda kukusanya fedha ili tuweze kuendesha taasisi hii vizuri.hatuwezi kusonga mbele bila kuwa na fedha za kutekeleza mikakati hio. Hata katika miradi ya maendeleo inataji fedha kwa ajili ya utekelezaji”
Kadhalika katika kikao hicho wajumbe walishauri ofisi ya Mkurugenzi kupitia idara ya Mipango na Ufuatiliaji kupitia changamoto zote zilizojitokeza kutoka kila kata na kuzitafutia ufumbuzi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa