• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Utawala
      • Biashara, Viwanda na Uwekezaji
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya jamii
      • Afya
      • Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Ujenzi
      • Fedha na Uhasibu
    • Vitengo
      • Manunuzi na Ugavi
      • Sheria
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Mawasiliano Serikalini
      • Tehama
      • Utamaduni, Sanaa na Michezo
      • Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
      • Usafi wa Mazingira na Udhibiti Taka
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Kilimo na Mifugo
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za kudumu
    • Ratiba ya kuonana na mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya picha na video za shughuli za maendeleo

Maendeleo ya Jamii

Idara ya Maendeleo ya Jamii ni idara kiungo kati ya jamii, Serikari na wadau mbalimbali wa maendeleo. Idara ya Maendeleo ya Jamii ina vitengo (Section) kama ifuatavyo:-

  • Sekta cha vijana
  • Sekta ya kudhibiti UKIMWI
  • Dawati la jinsia  
  • Sekta ya Uratibu wa shughuli za NGOs.

Kama Idara mtambuka idara hushirikiana na idara nyingine katika Halmashauri ya Wilaya  pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali na Asasi za kiraia zilizopo katika maeneo ya Wilaya hii.


          MAJUKUMU YA IDARA YA MAENDELEO YA JAMII.

Shughuli zinazotekelezwa  na idara hii ni pamoja na :-

  • Kuhamasisha jamii kubuni, kupanga, kutekeleza, kusimamia na kutathimini mipango na miradi yao ya maendeleo.
  • Kuelimisha jamii kuondokana na mila zenye zilizopitwa na wakati na kuwa na mtazamo wa kupenda mabadiliko chanya.
  • Kuhamasisha jamii juu ya matumizi ya teknolojia rahisi na sahihi kwa kutumia rasilimali  zilizopo na zinazopatikana kwa urahisi.
  • Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kutoa taarifa na matukio mbalimbali kama vifo, milipuko ya magonjwa, masoko, uzalishaji mali, vyakula, ajira na unyanyasaji wa kijinsia.
  • Kuratibu shughuli zote za maendeleo zinazosimamiwa na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) katika Wilaya.
  • Kufanya utafiti na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na matatizo mbali mbali yanayorudisha nyuma maendeleo katika jamii kwa kushirikiana na watumishi wa sekta zingine.
  • Kusimamia na kuratibu shughuli za maendeleo ya wanawake, vijana, watoto na wazee.
  • Kuhimiza, kujenga na kuimarisha ari ya kufanya shughuli za maendeleo kwa kujitolea katika maeneo yao.
  • Kueneza elimu ya uraia mwema kwa jamii
  • Kutoa elimu kwa jamii ili kuepukana na maambukizi  ya VVU/UKIMWI.
  • Kusimamia, kusambaza, kuelimisha jamii juu ya sera mbalimbali za maendeleo ya jamii kuanzia ngazi ya jamii.


         HUDUMA ZA KIJAMII

         Idara ya maendeleo ya Jamii inatoa huduma mbalimbali za kijamii kwa ajili ya kuhakikisha jamii inapata maendeleo inayoyahitaji:-

  • Kusajili vikundi vya vijana, wanawake na makundi ya mchanganyiko (wanawake na wanaume)
  • Kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa makundi mbalimbali ya wajasiriamali wadogo wadogo ili kuinua mitaji yao
  • Kutoa misaada kwa makundi maalumu (walemavu, watoto yatima, wajane, watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi)
  • Kusaidia wafungwa wa muda mfupi  kutoka gerezani na kupangiwa kazi za nje
  • Kutoa elimu ya kujitambua na afya ya uzazi kwa wanafunzi wa shule za sekondari
  • Kutoa msaada wa mitaji midogo midogo kwa makundi ya kijasiriamali ya watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI


      

Matangazo

  • Orodha ya Walioitwa kwenye Usaili September 20, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA KISHAPU November 21, 2025
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI

    December 22, 2025
  • RC MHITA AWATAKA MADIWANI KISHAPU KUDUMISHA USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO - NGUZO KUFANIKISHA MIPANGO YA MAENDELEO.

    December 19, 2025
  • DED JOHNSON ATOA MAELEKEZO MUHIMU KWA MADEREVA

    December 19, 2025
  • MKUTANO WA BARAZA LA MADIWANI WAMTEUA MWENYEKITI MPYA HALMASHAURI YA WILAYA KISHAPU

    December 03, 2025
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu: +255282770020

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa