Chimbuko la Wilaya ya Kishapu.
Wilaya ya Kishapu ilianzishwa mnamo Julai 1, 2002 kama matokeo ya mgawanyiko wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga. Mnamo Julai 1, 2006. Halmashauri ilianzishwa rasmi baada ya kutangazwa kutoka gazeti la Serikali la Julai 29, 2005 na Na. 220 ya GN. Wilaya ya Kishapu ni kati ya wilaya sita zinazounda mkoa wa Shinyanga ambapo wilaya zingine ni Kahama mjini,Ushetu,Msalala,Shinyanga vijijini na Shinyanga mjini. Wilaya ya Kiahapu inapakana na Wilaya ya Meatu (mkoa wa Simiyu) upande wa mashariki, Shinyanga vijijini na mjini upande wa magharibi, wilaya ya Maswa upande wa kaskazini na wilaya ya Igunga kwa upande wa Kusini.
Ukubwa wa Eneo.
Wilaya ina kilomita ya mraba 4,333 ambayo ni sawa na asilimia 8.5 ya eneo la Mkoa wa Shinyanga ambao una kilomita za mraba 50,781. Eneo la makazi ya binadamu ni kilomita ya mraba 1,536.4 sawa na asilimia 35.5 ya eneo la jumla la Wilaya. Eneo la shughuli za Kilimo ni kilometa za mraba 1,898.33 sawa na asilimia 43.8 ya eneo la jumla. Eneo la kutunza mifugo ni kilomita za mraba 747.02 sawa na asilimia 17.2 ya jumla ya eneo. Eneo la misitu ni kilomita za mraba 100.78 sawa na asilimia 2.3 ya eneo la jumla.Eneo lisilozalisha lina ukubwa wa kilometa 50.47 sawa na asilimia 1.2 ya eneo la jumla.
Eneo la Utawala na Watu wake.
Wilaya ina Tarafa tatu 3, kata 29 na Vijiji 117, Vitongoji 660 na jimbo moja la uchaguzi. Wilaya imefanikiwa kuanzisha Mamlaka mji mdogo wa Kishapu. Idadi ya watu katika sensa ya mwaka 2022,wilaya ilikua na idadi ya watu 335,483.
Hali ya hewa.
Wilaya ya Kishapu hupata wastani wa joto la nyuzi 28 C na mvua kati ya 450-900mm kwa mwaka. Wilaya hupata msimu mmoja wa mvua ambao huanza katikati ya mwezi Novemba hadi mwanzoni mwa mwezi Januari, ukifuatiwa na kipindi cha ukame kuanzia katikati ya Januari hadi mwishoni mwa mwezi Februari. Mvua hunyesha tena mwezi Machi na kuishia Mei.
Shughuli za kiuchumi.
Wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu hujihusisha na shughuli za Kiuchumi kama ifuatavyo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa