Katika Uchaguzi mkuu wa Rais, Ubunge na Udiwani wa Oktoba 28, 2020 Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka kidedea katika ngazi ya Ubunge Jimbo la Kishapu.
Matokeo hayo yametangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kishapu Emmanuel Johnson leo Oktoba 29 ambapo Boniphace N. Butondo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ameibuka kinara kwa idadi ya kura 54, 864 kutoka katika kata zote 29 za jimbo la Kishapu, huku Idd Salum Amri wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akifuatia kwa kupata kura 9,903.
Msimamizi huyo amempongeza Mbunge huyo huku akimtakia mafanikio mema katika kulitumikia taifa na kutatua kero za wananchi wa Kishapu.
“Kwa mamlaka niliyopewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Namtangaza Mheshimiwa Boniphace Butondo kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge mteule wa Jimbo Kishapu katika uchaguzi uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020” Amesema Johnson alipokuwa akimtangaza mbunge huyo.
Katika uchaguzi huo idadi ya wapiga kura walioandikishwa ni 155,785, huku idadi halisi ya wapiga kura ikiwa ni 66,422, idadi ya kura halali ikiwa ni 64,764na idadi ya kura zilizokataliwa ni 1,655.
Naye Mshindi wa uchaguzi huo Mheshimiwa Boniphace Butondo amewashukuru sana wananchi wote waliomchagua kuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu na kuahidi mara maada ya kuapishwa na kuwa mbunge ramsi atawatumikia kwa moyo mmoja.
“Nawashukuru kwa moyo wangu, wote waliojitokeza kupiga kura na kunichagua katika nafasi hii. Mmeonyesha upendo wa hali ya juu kwangu, naahidi kurudisha fadhila hizi kwa kuwatumikia ipasavyo. ”amesema Mheshimiwa Butondo.
Aidha katika uchaguzi huo nafasi za Madiwani katika kata zote 29 za Jimbo la Kishapu zimechukuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa