Vijiji vya Shagihilu na Ndoleleji katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu vinatarajia kunufaika na miradi ya maji yenye thamani ya jumla ya sh. milioni 510 zilizotolewa na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga ametembelea miradi hiyo miwili inayoendelea kutekelezwa katika vijiji vya Shagihilu na Ndoleleji kata ya Shagihilu.
Mradi wa Shagihilu una thamani ya sh. milioni 464 na wa Ndoleleji wenye thamani ya sh. milioni 46 yote inatarajiwa kunufaisha wananchi kutoka vijiji hivyo kupitia Programu ya Maji.
Akitoa taarifa ya maendeleo ya miradi hiyo Mhandisi wa Maji, Lucas Said alisema ujenzi wa miradi hiyo inajumuisha mashine ya kuvuta maji kutoka kwenye chanzo na ujenzi wa tangi la kuyahifadhi.
Alisema kuwa pia kiasi hicho cha fedha kinatarajiwa kutumika katika hatua ya usambazaji wa maji pamoja na ujenzi wa vituo vya kuchotea maji kwenye kijiji husika ili kuwafikia wananchi.
Katika ziara hiyo aliambatana na watendaji kutoka Halmashauri wakiwemo Mhandisi wa Maji Wilaya, Lucas Said, Afisa Mipango Wilaya, Mang’era Mang’era, Afisa Elimu Msingi Ufundi, Moshi Balele na Mhandisi kutoka Idara ya Maji, Dagadaga Lucas.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa