Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaagiza wakuu wa mikoa kuhakikisha halmashauri zote zinatenga maeneo kwenye vijiji yatakayotumika kwa ajili ya shughuli ya kuhifadhi misitu.
Dkt. Kigwangalla alitoa agizo hilo leo wakati wilayani Kishapu wakati akihitimisha kilele cha maadhimisho ya Upandaji Miti kitaifa ambapo alivitaka vijiji hivyo kuunda kanuni na taratibu za kusimamia maeneo hayo.
Sambamba na hilo aliugiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuchagua mikoa 10 itakayotakiwa kuanza utekelezaji wa agizo hilo kwa kuanzia na Shinyanga, Tabora na mingineyo inakabiliwa na uharibifu wa misitu.
Pia alitoa siku saba kwa TFS kuandaa mpango wa namna ya kushirikiana na uongozi wa vijiji kupanga maeneo yanayotakiwa kuhifadhiwa misitu wa uhifadhi wa misitu katika maeneo hayo.
“Natoa siku saba kwa TFS kuwasilisha kwangu mpango wa tathmini ya uvunaji wa mazao ya misitu nchi nzima kwa kuzingatia rasilimali za misitu kilichopo pamoja na kiwango halisi kitakachotakiwa kuvunwa ambacho hakitazidi robo ya rasilimali iliyopo,” alisema.
Katika hatua nyingine Dkt. Kigwangalla alitoa siku 30 kwa wananchi waliovamia ngitiri waondoke mara moja vinginevyo wataondolewa kwa nguvu huku akisisitiza wananchi wajifunze kilimo na ufugaji usioharibu mazingira.
Aliagiza kila mwananchi apande miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kutokana na hali hiyo kiwango cha mvua kimepungua kutokana na vitendo hivi vinavyofanywa na binadamu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa