Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa katika miti 100 iliyopo ni kumi pekee ndiyo iliyopandwa wakati 90 ni ya asili iliyojiotea yenyewe.
Dkt. Kigwangalla amesema hayo jana wakati akizungumza kwenye kilele cha Maadhimisho ya Upandaji miti kitaifa kwenye viwanja vya Shirecu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Alisisitiza kuwa ni jukumu letu sote kuchukua hatua ya kupanda na tuachane vitendo vya ukataji ili kuepusha hali ya jangwa na tunapaswa kuhifadhi miti tuliyonayo kwanza.
Alitahadharisha kuwa takwimu hizi zinashtua na kuwa tuko katika hali mbali ya na hivyo tu kazi kubwa ya kufanya hivyo tunahitaji tupande miti kwa wingi ili kurudisha hali ya misitu.
Alisema mabadiliko ya tabianchi yanasababisha changamoto mbalimbali zikiwemo upungufu wa mvua kutokana na vitendo vya ukataji kiti katika maeneo mbalimbali nchini.
“Uharibifu wa mazingira unakua kwa kasi kubwa ndani ya muda mfupi na tusipoangalia tutakosa chakula ndugu zangu tuna kazi kubwa ya kufanya na kazi hiyo ni kupanda miti,” alisisitiza.
Awali akiwasilisha taarifa ya maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Ezekiel Mwakalukwa alisema tafiti zinaonesha nchi inapoteza ekari 372,000 za miti kila mwaka.
Alisema hali hiyo husababisha upungufu mazao ya misitu kwa takriban mita za ujazo milioni 19.5 za ujazo na ili kuziba pengo hilo tunatakiwa kupanda miti 185,000 ambazo ni sawa na milioni 280 kwa mwaka kwa kipindi cha miaka 17 mfululizo.
Dkt. Ezekiel alisema kuwa tatizo la ukame lililoanza kuikumba baadhi ya mikoa hapa nchini ikiwemo Dodoma, Shinyanga, Tabora limetokana na mabadiliko ya tabianchi.
Alisema kuwa Serikali ilianza kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na hali hiyo zikiwemo kufanya kampeni, makongamano na semina ili kutoa elimu kwa wananchi tangu miaka ya 1980.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa