Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imekabidhi vyumba vitatu vya madarasa kwa Shule ya Sekondari Mwadui Ufundi baada ya umaliziaji wakekukamilika.
Ukarabati huo wa vyumba hivyo vya madarasa vilivyogharimush. milioni 10.9 ni matokeo ya Mradi wa Lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) wenyekulenga kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi mradi huo, Mwakilishi wa Mkurugenzi waHalmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Veronica Massawe alipongeza Bodi ya Shule nauongozi wake kwa usimamizi mzuri wa ujenzi.
Alisema panapokuwa na usimamizi mzuri wa miradiunafanya watoaji fedha za miradi kujenga imani na wanaowapa fedha hizo na hivyokuendelea kusaidia kuboresha sekta hiyo.
Aliongeza kuwa mradi huo utaweza kutoa tija kwakuleta ufanisi katika ufundishaji ambapo madarasa hayo yataweza kuwahudumiawanafunzi shuleni hapo.
Aidha, Veronica ambaye pia ni mchumi waHalmashauri ya Wilaya hiyo alisisitiza ushirikiano baina ya walimu na wanafunziambao ndio kichocheo ya mafanikio.
Alisema kuwa ufanisi na matokeo mazuri hutokana nawalimu kuwa na ushirikiano mzuri na wanafunzi wao hasa katika kuhakikishawanawapa maarifa.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa