Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa jumla ya vitabu 50,100 kwa ajili ya shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
Vitabu hivyo vya ziada, kiada na mihtasari ya masomo anuai vya vimelenga kuboresha sekta ya elimu.
Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sostenes Mbwilo amesema msaada huo ni sehemu ya mpango wa elimu bila malipo unaotekelezwa na Serikali kwenye shule za msingi na sekondari.
Akipokea msaada huo Mbiwlo aliishukuru Serikali na kusema utakuwa chachu ya kuboresha sekta hiyo.
"Tumeanza kusambazwa vitabu mashuleni na kama unavyoona walimu wakuu wameanza kuvipokea kwa ajili ya kutumika katika vituo vyao," alisema.
Aidha Afisa Elimu huyo aliwataka walimu wakuu hao kuvitumia kama ambavyo inatakiwa ili kuendelea kuboresha elimu wilayani humo.
Huu ni mkakati wa Serikali kuhakikisha sera ya utoaji wa elimu iliyo bora inafanikiwa nchini kote.
Itakumbukwa pia hivi karibuni ilitoa vitabu vya kujifunzia na kiongozi kwa walimu katika Halmashauri hiyo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa