Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 kiasi cha shilingi bilioni 39,614,341,468.12 ambazo ni malipo ya mishahara ya watumishi ndani ya halmashauri, miradi ya maendeleo na mengineyo leo Februari 2021 katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu.
Katika bajeti hiyo ya fedha imejikita kuwa ya uwazi na uwajibikaji kwa watumishi pamoja na wananchi ili kuinua maendeleo ya ndani ya halmashauri ya wilaya hiyo ambapo fedha hiyo zaidi ya bilioni 39, mapato ya ndani pekee ni bilioni 2,810,935,300.
Akifafanua bajeti hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson amesema elimu bila malipo bilioni 1,853,459,500, ruzuku ya mishahara bilioni 25,259,231,814 na miradi ya maendeleo ni bilioni 9, 767,449,055.
Wakichangia bajeti hiyo ya mwaka wa fedha madiwani wa baraza hilo akiwemo Diwani wa Kata ya Songwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Abdulkadir Ngoromole amesema ni wajibu wa kila diwani kuhakikisha anasimamia mikakati ya bajeti ili fedha hiyo iweze kutumika kama ambavyo imetarajiwa ndani ya halmashauri.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Nyabaganga Taraba amewataka madiwani wa halmashauri hiyo kushirikiana na halmashauri kuendeleza mchakato wa kukusanya mapato kupitia vyanzo vya mapato.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa