Jumla ya makarani waongoaji wa uchaguzi 181 Jimbo la Kishapu mkoani Shinyanga wameapishwa leo Oktoba 24, 2020 katika kituo cha Shirecu wilayani humo na kupewa semina tayari kwa ajili ya uchaguzi mkuuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28, mwaka huu.
Makarani hao wameapishwa na Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kishapu Emmanuel Johnson ,ambapo wakati akitoa semina na viapo kwa makarani hao amewaasa kulinda siri zinazohusu uchaguzi huo, huku akisisitiza kulinda amani ya nchi kwa kufanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria na kanuni za uchaguzi.
“Hampaswi kutoa matokeo ya uchaguzi kwa mtu yeyote asiyehusika, kama kuna jambo lolote mnapaswa kutoa taarifa kwa tume kulingana na taratibu zilizowekwa” amesema
Naye Afisa Uchaguzi Msaidizi wa Jimbo la Kishapu, Deus Ngelanizya amewashauri maafisa hao waelekezaji kuwa baada ya kuapishwa wamekuwa watumishi wa Tume (NEC) hivyo siku ya uchaguzi hawapasi kuonyesha msimamo wa vyama vya siasa.
Ngelanizya pia amewataka kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu wakati wa upigaji kura ambao ni wazee, akina mama wajawwazito na watu wenye ulemavukwa kuwaelekeza na kuwasaidia vifaa mbalimbali vya kupigia kura.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa