Elimu ya afya juu ya kujikinga na ugonjwa wa Homa ya Mapafu unaosababishwa na Kirusi aina ya Corona imetolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kupitia Timu ya Majanga ya Afya Wilayani humo. Elimu hio imetolewa kwa mama lishe pamoja na wana jamii wote wakiwemo wafanya biashara sokoni, wauza nyama leo tarehe 18 March 2020 katika kata ya Maganzo wilaya Kishapu mkoani Shinyanga.
Akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Afya wa Wilaya ya Kishapu Erick Yossam Muhigi amewataka mama lishe pamoja na ana jamii wote katika kata ya Maganzo kujua hali ya afya zao kwa kupima na kuwa wasafi muda wote kwani wanahudumia watu wengi katika biashara zao.
“Hakikisha unapimwa kila baada ya miezi mitatu na unapewa na risiti, kila mtu avae sare kuanzia kofia, aproni na viatu vya kufunika pamoja na wahudumu wake wote, weka ndoo ya maji ya moto yenye koki, sabuni ya maji juu ya ndoo na tishu, weka hand sanitizer yenye mchanganyiko wa spirit na glycerine, ambapo chupa yenye ujazo wa lita moja changanya vifuniko viwili vya glycerine yatari kwa matumizi, nawa mikono mara kwa mara, vaa masks inayofunika pua na mdomo kwani mnaongea na watu wengi sana, vyombo vyote vioshwe kwa maji ya moto na hakikisha ni visafi muda wote, hakikisha una chombo chenye mfuniko kwa ajili ya kuhifadhia takataka, epuka kuwa na kucha ndefu na rangi kwenye vidole vya mikono, epuka kuweka watoto na ndugu wenye umri mdogo, kwenye biashara zako” alisema Muhigi
“Endapo utapatikana na kosa moja faini ni shilling elfu kumi, na endapo utalipa faini hakikisha unapewa risiti. Ukishindwa kulipa faini tunachukua vyombo vyako vyote vya biashara na tutakaa navyo kwa miezi mitatu, endapo utashindwa kuvikomboa vitauzwa kwa ajili ya fidia” aliongeza Muhigi.
Katika hali hio Halmashauri imetoa siku mbili kwa ajili ya Mama Lishe wote katika kata hio kupima afya zao ambapo wataanza tarehe 21 na 22 March 2020.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa