Jeshi la Polisi Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga limepokea gari jipya kwa ajili ya matumizi ya shughuli zake kutoka mgodi wa almasi wa Mwadui.
Gari hilo aina ya Nissan Hilux lenye thamani ya sh. milioni 80 limepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack ambaye alikabidhi jeshi hilo.
Akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya gari hilo yaliyofanyika wilayani humo Mhe.Telack aliushukuru mgodi kwa msaada huo.
Telack ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa alisema kuwa gari litawezesha shughuli za Polisi kufanyikaa kwa ufanisi.
Aliwaomba wasichoke kuendelea kuisaidia Kishapu pamoja na kushirikiana na Serikali ya wilaya hiyo kwani wao pia ni sehemu ya jamii hiyo.
Aidha alilitaka jeshi hilo kulitumia gari hilo walilokabidhiwa kwa matumzi yaliyokusudiwa ya kulinda wananchi ili waendelee kuwa na imani nalo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa