Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe Zainab Telack amezindua maadhimisho ya upandaji miti kitaifa yanayofanyika katika viwanja vya Shirecu wilayani Kishapu kwa muda wa siku tatu.
Mhe. Telack akiwa na mgeni wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Mhe. Aggrey Mwanri wote kwa pamoja wametaka pawepo na urahisi wa upatikanaji wa nishati mbadala vijijini ili wananchi wapunguze matumizi ya mkaa.
Wametoa rai hiyo kwa nyakati tofauti wakati wa maadhimisho ya upandaji miti kitaifa yanayofanyika wilayani Kishapu ambapo yameambatana na zoezi la upandaji miti katika vijiji vya Mwatuju na Songwa.
Walisema kuwa pakiwepo na nishati mbadala wananchi wataepuka matumizi ya mkaa na kuni kutokana na vitendo vya ukataji miti katika misitu yetu na hivyo kuifanya iendelee kustawi.
Mhe. Telack kwa upande wake alisema kuwa sehemu kubwa ya wananchi husasan katika maeneo ya vijijini hawana nishati mbadala wa kuni na mkaa hivyo hulazimika kukata miti ovyo.
Aidha, aliziagiza Halmashauri zote zilizopo katika Mkoa wa Shinyanga kutunga sheria ndogo ambayo itawezesha kuwachukulia hatua wanaoharibifu wa misitu kwa ukataji na uchomaji miti.
Aliongeza kwa kusema Wilaya ya Kishapu inakabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua nah ii ni kutokana na ukataji miti unaofanywa na wananchi wenyewe hali inayosababisha kuwepo kwa ukame.
Aliagiza wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ukataji miti kiholela wakamatwe na kuchukuliwa hatua kali za kisheria ili tabia hiyo ikome na kuifanya Kishapu na mkoa kwa ujumla kuwa ya kijana.
“Tupunguze kukata miti na inasikistisha sana kuona mtu ana mti mmoja halafu anaukata kwa panga nasisistiza wananchi tulikatae hilo tumeambiwa mti ni uhai tukikata miti mvua haitanyesha na hiivyo tutakosa chakula na itasababisha kukosa uhai,” alisema.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa