Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imezindua zoezi lakunywesha dawa za magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele ya kichocho na minyootumbo katika shule za msingi 122.
Zoezi hilo limezinduliwa rasmi leo Julai 5, 2018 na Mkuuwa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba katika Shule ya Msingi Kanawa kataya Ukenyenge.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo, Mhe.Taraba aliwataka wazazi kuwapeleka watoto wao wenye umri wa miaka mitano hadi14 kwenye vituo vinavyotoa huduma hiyo ili wapate kinga.
Alisema kuwa watoto wanapopata kinga ya magonjwa hayotunapunguza gharama ambazo zingetumika katika kuwapatia matibabu na hivyojitihada zote zinakuwa ni bure pasipo na maafanikio.
Mhe. Mkuu wa Wilaya aliongeza kuwa tangu kuanza kwazoezi hilo limefanikiwa kwa kiwango cha juu hivyo kufanya jitihada zakuyatokomeza mago njwa kufanikiwa.
“Ndugu zangu tangu tuanze zoezi hilo kwa mwaka wakwanza tulifanikiwa kwa asilimia 95, mwaka wa pili kwa asilimia 97 na mwaka huutunategemea kufika asilimia 100 na zaidi,” alisisitiza.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa