Wakulima wa zao la pamba wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga wameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kupitia uongozi wa Halmashauri ya Wilaya a Kishapu kwa kuwapatia kwa mkopo dawa za kuulia wadudu waharibifu ambapo kwa sasa wataepukana na mikopo umiza waliyokuwa wakitozwana watu binafsi.
Shukrani hizo zimetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wanachama wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha Kishapu (AMCOS) wilayani Kishapu wakati wa uzinguzi wa ugawaji wa viutilifu vilivyotolewa kwa mkopo na Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) Kanda ya Magharibi.
Wakulima hao walisema uamuzi wa serikali kuwapatia dawa za kuulia wadudu kwa njia ya mkopo utaongeza ufanisi katika shughuli zao za kilimo na hawatahangaika tena kutafuta viuatilifu hivyo kutoka kwa watu binafsi wanaowatoza riba kubwa na kusababisha washindwe kunufaika na kilimo chao.
Mmoja wa wakulia hao, Ally Mfaume alisema kitendo cha serikali kuwakumbuka wakulima kwa kuwapatia viuatilifu hivyo itawasaidia wakulima kuepuka changamoto ya pembejeo hivyo watapulizia dawa mapema katika pamba zao tofauti na msimu uliopita.
“Mwanzo tulikuwa tunaingia mkataba na wafanyabiashara binafsi kwa sharti bada ya mavuno kuwalipa pamba mbegu, kwa mfano mtu unapewa gunia mbili za pamba sawa na kilo mia moja kalini ukivuna unatakiwa umpatie aliyekukopesha kilo mia mbili za pamba”
“Kwa kweli tulikuwa tunapata hasara, kilo mia mbili ni nyingi sana, ukizipunguza kwenye mavuno yako mkulima unajikuta unapata hasara. Lakini kwa utaratibu huu wa kukopeshwa na serikali tutaepukana na mikopo kandamzi, na tunaomba hii huduma iwe endelevu, maana uwezo wa kulipa tunao” alieleza Mfaume.
Akwa upande wake mgeni rasmi katika ugawaji wa viuadudu hivyo, David Isanga aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Taraba amewatahadharisha viongozi wa Kishapu AMCOS kutofanya udanganyifu wa aina yoyote katika zoezi la ugawaji wa viuadudu hivyo kwa wakulima.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa