Wauguzi wilayani Kishapu wameshauriwa kujenga utamaduni wa kujiendeleza kielimu ili kuweza kupanua wigo katika kutoa huduma yaafya kwa wananchi.
Mwito huo umetolewa leo Aprili 12, 2018 na AfisaTarafa ya Kishapu, Given Noah akimwakilisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Nyabaganga Taraba wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani.
Noah alisema kuwa wauguzi wana nafasi kubwa yakutumia wakati huu kujiunga na vyuo vinavyotoa elimu ya afya ngazi za juu nakujiongeza ujuzi wa kazi.
Aliwataka watumishi hao wa afya kutosubiri na kuzeekawanapaswa kuchangamkia fursa zinazotolewa na hata kujisomesha wenyewe bilakuogopa gharama za masomo.
“Niwashauri wauguzi msiache kutumia muda huuhuwezi kujua kuna siku watastaafu watumishi au vituo vingie vya afya vinaanzishwasasa wewe kama umesoma kwa ngazi ya juu unaweza kuchukua nafasi,” alisema.
Aidha watumishi wa afya wanaopata elimu ngazi yajuu kuacha kutumia kauli mbaya kwa wenzao ambao wamewazidi elimu hali inayowezakuleta chuki na mifarakano.
Pamoja namambo mengine aliwataka watumishi kuzingatia viapo vyao, kanuni na taratibu zakiutumishi na kuwa Serikali inalenga kutatua kero zao inapobidi.
Afisa Tarafa huyo alisisitiza kuwa wauguzi ni kiungomuhimu katika kutimiza azma ya Serikali katika kuboresha huduma mbalimbalihususan za afya katika maeneo mbalimbali nchini.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa