Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu ikishirikiana na Shirika la Misaada ya Kijamii (REDESO) imekabidhi hati 43 za kimila za ardhi kwa wananchi katika kijiji cha Negezi kata ya Ukenyenge.
Hati hizo zimekabidhiwa na Katibu Tawala Wilaya ya Kishapu, Shadrack Kengese kwa wananchi hao ikiwa ni sehemu ya jumla ya hati 87 ambazo zinatarajiwa kutolewa katika kijiji hicho.
Kengese aliwataka wananchi hao kuzitumia hati kwa kuboresha hali zao kiuchumi kwa kukopa katika taasisi za kifedha na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo na kujipatia kipato.
Alisisitiza kilimo chenye tija katika ardhi hizo ambapo aliwataka kufuata kanuni bora za kilimo ili kupata mavuno kwa kiasi kikubwa ambapo wataipa thamani ardhi wanayomiliki.
Aidha, alisema pamoja na hayo pia wananchi wanapaswa kupanda miti ili kutunza mazingira kwani ardhi iliyotunzwa kwa kupandwa miti ina thamani kubwa zaidi ya ile isiyokuwa na mti hata mmoja.
Kwa upande mwingine Katibu Tawala huyo aliwataka wananchi waliokabidhiwa hati hizo kuwahamasisha wanajamii wenzao kuona umuhimu wa kupata hati za kimila za kumiliki ardhi katika maeneo yao.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa