Halmashauri ya Wilayaya Kishapu imetajwa kuwa ni miongoni mwa Halmashauri tisa vinara katika utoaji habari kupitia tovuti zao kwa wakati.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembeamesema hayo Machi 12 jijini Arusha wakati akifungua mkutano mkuu wa mwakawa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini unaoendelea katika Ukumbiwa AICC.
Dkt. Mwakyembe alizitajaHalmashauri nyingine zinazofanya vizuri ni pamoja na Manispaa ya MtwaraMikindani, Mufindi, Kibaha, Mlele, Kinondoni, Ilala pamoja na Ubungo.
Kwa upande wa Sekretarietiza Mikoa ni pamoja na Mwanza, Mara, Kagera, Tabora, Shinyanga, Simiyu, Arusha,Tanga, Lindi, Mtwara,Ruvuma, Rukwa, Mbeya, Iringa, Morogoro, Geita, Katavi naSongwe.
Aliongeza kuwa Serikalikupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ilizinduatovuti za Mikoa na za Halmashauri ili kuongeza uwazi na uwajibikaji wa Serikalikwa wananchi wake.
Itakumbukwa katikaufunguzi iIlisisitizwa kuwa tovuti hizo zilenge kuwa majokofu ya habari na si magofuili kumpa mwananchi habari zinazohusu Serikali katika maeneo mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa