Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu imetoa Sh. Milioni 6.4 kwa kikundi cha watu wenye ualbino wilayani humo kwa ajili ya kuendeleza mradi wa maji safi na salama.
Afisa Maedneleo ya Jamii wa Wilaya hiyo, Joseph Swalala amesema kuwa fedha hizo zinatokana na sehemu ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Swalala alisema kuwa fedha zilizotolewa kwa kikundi hicho zitawezesha upatikanaji wa maji na kipato kwa watu wenye ualbino kupitia mradi huo kwa njia ya machujio.
Alibainisha kuwa mradi wa kikundi hicho ulioanzishwa rasmi mwaka 2017 una lengo la kuelimisha jamii kuondokana na mila potofu ya watu wenye ualbino pamoja na kuinua pato lao.
Afisa Maendekeo ya Jamii huyo aliongeza kuwa Halmashauri itaendelea kuwasaidia kupata mikopo ili waweze kuanzisha miradi mingi zaidi ya ya maendeleo na kuinua kipato chao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania (TAS) Wilaya ya Kishapu, Seif Rashid alisema watu wenye ualbino wameanza kuonekana ni kuwa na umuhimu.
Kutokana na hilo kikundi hicho kinajihusisha na shughuli mbalimbali za maendeleo wilayani Kishapu.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa