Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe Sophia Edward Mjema amewashauri wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuanza kujiandaa kwa kilimo msimu wa mwaka 2022/2023 kwa kulima mazao yanayostamili ukame ili kwenda sambamba na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi kama ilivyo tolewa taarifa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini .
Mhe, Mjema ametoa ushauri huo wakati wa kikao cha maafa cha mkoa wa Shinyanga kilichokutana kupanga mikakati ya kukabiliana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi pamoja na kuangalia bei ya bidhaa na kufuatilia.
Hata hivyo mkuu wa mkoa amesema mkoa wake unaziada ya chakula na kutoa wito kwa wananchi kutunza chakula hicho japo kuwa kumekuwepo na tatizo la bidhaa za vyakula kupanda bei
Kwa upande wake Katibu tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Ndg, Berda Chamatata amesema mkoa wa Shinyanga unakadiliwa kuwa na Watu milioni 1,993,589 na mahitaji ya chakula tani laki 472,979 na uzalishaji wa msimu uliopita wa mwaka 2021/2022 ni tani laki 484,501 .
Kaimu meneja na wakala wa hifadhi ya chakula mkoa wa Shinyanga Ndg, Joseph Maige amesema wana chakula cha kutosha kwenye hifadhi yao kwa ajili ya mikoa 8 kwenye kanda yao huku meneja wa TMA Mkoa wa shinyanga Amesema msimu huu mvua ni chini ya Wastani.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa