Afisa Elimu msingi Wilaya ya Kishapu Ndugu, Angasilini O. Kweka Leo Amefungua Semina ya Siku 3 kwa Maafisa Elimu kata 29 na wakuu wa shule za msingi 60 kwajili ya Mafunzo elekezi ya Uthibiti bora wa shule wa ndani.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku 3 katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Kishapu.
Afisa Elimu baada ya kufungua semina hiyo aliwaasa maafisa Elimu kata na wakuu wa shule kwa kuwakumbusha majukumu yao ya kazi.
"Kwanza kabisa lazima tutambue sisi ni Walimu,na Ualimu ni kipaji ambacho Mungu ndiyo katupatia kwa hiyo lazima tuwajibike kwenye majukumu yetu na lazima kabisa sisi ndiyo tuwe wa kwanza kujithibiti, Pamoja na kutambua sisi ni walimu wajibu wetu ni kufundisha, wajibu wetu ni kuandaa Viongozi, kuandaa jamii yenye maadili na hili ni juku letu sisi Walimu.” Afisa Elimu alisema
Pia alitumia furusa hiyo kuwashukuru Maafisa Elimu kata na walimu wakuu kwa kufika kwa wingi kwenye Semina hiyo na amewaomba kushiriki vyema mafunzo hayo kwa sababu yana tija kubwa kwao.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa