Rais Samia Aipongeza Halmashauri ya Kishapu kwa Usimamizi Mzuri wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu kwa kazi nzuri waliyoifanya katika usimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024.

Salamu hizo ziliwasilishwa leo Machi 18, 2025 na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Ndugu Emmanuel Johnson, alipokuwa akizungumza na watumishi wa halmashauri hiyo katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri.

"Tulikuwa kwenye kikao cha ALAT Taifa, ambapo Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewapongeza sana watumishi waliopo Serikali za Mitaa, wakiwemo watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, kwa usimamizi mzuri wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024. Pia, Mhe. Rais ametutaka tuendelee kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano mkubwa, huku tukiendelea kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali," alisema Ndugu Johnson.

Aidha, Mkurugenzi huyo alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi na watumishi wote wa Kishapu kujihadhari na ugonjwa wa Mpox. Aliagiza Mganga Mkuu wa Wilaya kutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya ugonjwa huo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa