Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Peter Masindi amewataka Wananchi wa Kishapu kutumia nishati mbadala ili kupunguza kasi ya ukataji wa miti.

Ametoa tamko hilo leo tarehe 11 Machi 2025 wakati akizungumza na Wananchi wa Kata ya Maganzo katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Soko la Maganzo

Akizungumza wakati wa Mkutano huo, mhe. Masindi ametoa wito kwa wananchi kuungana katika kutunza na kulinda mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi zinazoathiri mazingira na uchumi katika Wilaya ya Kishapu

“Ndugu zangu lengo kubwa la katazo la matumizi ya kuni na mkaa kwa Wananchi ni kusonga mbele katika kudhibiti uharibifu wa mazingira, ukataji miti hovyo ambayo inasababisha hata mvua kuwa chache katika Wilaya ya Kishapu, maelekezo haya nayatoa kwa Wananchi wote, wanatakiwa kutunza mazingira na kuacha kukata miti ovyo," amesisitiza.

Aidha, Mhe. Masindi amewataka Wananchi wanaotumia kuni na Mkaa kucha mara moja na kujikita katika matumizi ya Nishati safi kwa kununua hata Mitungi Midogo ya Gesi

Aliongeza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kujipambanua katika suala zima la mazingira kwa kutekeleza miradi ya kujali mazingira.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu: +255282770020
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa