Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. BaloziSeif Ali Iddi leo amekabidhi kiti maalumu cha matibabu ya meno na vifaa vingine kwa Hospitali ya Wilaya ya Kishapu.
Mhe. Balozi Seif ambaye pia ni mlezi wa Chama ChaMapindunzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga ametoa msaada huo sambamba na viti vya magurudumu, makoti ya madaktari, fimbo maalumu za walemavu na wazeepamoja na ‘gloves’.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo, BaloziSeif alitoa rai kwa wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao badala yakusubiri hadi wapate magonjwa.
“Ni muhimu wananchi mkatambua afya zenu kwa kupimamagonjwa kama kisukari, presha na Virusi Vya Ukimwi ili kupata tiba mapema nakuongeza umri wa kuishi,” alisisitiza.
Aidha, aliwataka wananchi kutumia hospitali yawilaya kupata matibabu kwa kuwa wapo wataalamu watakaowahudumia badala yakwenda kupata huduma hiyo mbali.
Makamu wa Pili wa Rais aliongeza kuwa hospitalihiyo kupata kiti hicho maalumu cha matibabu ya meno kutasaidia kutibu zaidimeno badala ya kung’oa kama ilivyozoeleka hapo awali.
Balozi Seif alisema kuwa Serikali ya Mapinduzi yaZanzibar (SMZ) pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano zinafanya kazi kubwakwa pamoja kuwahudumia wananchi wote.
“Tunafanya kazi kwa pamoja kwa mujibu wa ilani nanje ya ilani ili kutatua matatizo ya wananchi wetu na ndio maana nimetoa zawadihizi ili kuwasaidia wananchi wote bila kuajali itikadi za kisiasa, hivyo msiogopekuja hapa kupata huduma za afya,” alisema.
Awali akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe.Zainab Telack alimshukuru kwa msaada huo akiwa kama mlezi na kumuomba aendeleena moyo huo huo pindi atakapopata nafasi.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa