• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

BALOZI WA PAMBA NCHINI TANZANIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA

Posted on: January 9th, 2023

Balozi wa Pamba nchini Tanzania msimu wa mwaka 2022-2023 Bwana Agrey Mwanri amesema hata sita kuwachukulia hatua viongozi ambao hawatatimiza wajibu wao wa kusimamia wakulima wa zao la pamba kulima kwa kufuata sheria katika maeneo yao katika kamati teule ya waziri wa kilimo ya zao la pamba.


Mwanri amesema hayo leo Januari 9, 2023  katika kikao kazi maalum cha kujengeana uwezo kilichowakutanisha watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji,maafsa ugani pamoja na baadhi ya watumishi wa serikali ngazi ya halmashauri na wilaya katika ukumbi wa Shirecu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.


“Wakati mwingine kutowajibika kwenu vizuri kunapelekea wakulima kulima kiholela, zao la pamba lipo kwa mjibu wa sheria za nchi na sio kienyeji sheria no.2 ya mwaka 2001 na ile ya 2011 zilitungwa kanuni 10 moja wapo ya kanuni inamtaka kila mkulima kung’oa na kuchoma maotea yoote ya msimu uliopita ili kuua wadudu waharibifu kuhamia kwenye msimumpa,kupanda kwa msitari pamoja na kupulizia dawa ya kuuwa wadudu”


Ameongeza kuwa wilaya ya kishapu na maswa kata ya Itilima bado kunauelewa mdogo juu ya kulima kilimo chenye tija jambo lililopelekea waanzishe kuwepo mkulima mwezeshaji ambae atakuwa ni chambo kwa wakulima wengine,kutoa elimu ya kutosha huku akiwaasha viongozi wawe mfano katika zao hilo kwa kwa kufanya hivo kutainua na kuongeza pato la mtu mmoja na taifa ikilinganishwa na mwaka 2021-2022.


Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ugawaji na usambazaji viuadudu na vinyunyizi Bw Joseph Bukalasa alisema kamati hiyo yenye watu 10 kutoka taasisi mbalimbali za serikali imeundwa kwa maelekezo ya waziri wa kilimo Mhe. Husein Bashe yenye lengo la kudhibiti na kuzuia uchepushaji wa upotevu pamoja na udhibiti ubora baada ya kupokea kutoka kwa mdhabuni kwenda kwa mkulima.


Aidha katibu tawala wa wilaya ya Kishapu Bw Shadrack Tengese alisema kuwa ukosepfu wa uadilifu katika kazi unapelekea uzembe ndani ya baadhi ya vyama vya msingi na kusababisha washindwe kufikia malengo yaliyokusudiwa katika zao hilo la pamba.


“Kwa bahati mbaya mikataba haioneshi kama kiongozi wa amkosi akikosea atawajibika vipi mdhamini wake japo tutafika tuendako, maafisa ugani tusimamie kanuni za kilimo kwenye maeneo yetu iwapo wakulima kila siku wanamwaga mbegu na wewe uko pale je unastahili kuwepo pale? Kila mtu akisimamia kazi yake vizuri tutakuwa tumemsaidia Mhe. Raisi kufikia malengo yale ambayo amekusudia katika sekta ya kilimo. ndugu zangu yamkini nimesema kwa ukali lengo hapa ni kumtaka kila kiongozi kutimiza wajibu wake”


Hata hivyo wake afisa uchunguzi wa kuzuia na kupambana na rushwa kutokea jijini Mwanza Bw Protas Henry ambae pia ni mjumbe wa kamati ya usambazaji pembejeo alisema kuwa lengo la serikali ni kuinua zao la pamba na wataalamu wamethibitisha kwa mkulima atakaefanya vizuri na kuzingatia kanuni mavuno yataongezeka


“Lengo la serikali msimu wa 2022-2023 ni kuzalisha tani 500000 kutoka tani 17300 Kishapu inatakiwa kuzalisha jumla ya tan 50,000 na hili tutafanikiwa baada ya wakulima kulima mapema,kupalilia na viuwadudu na vinyunyizi kufika kwa wakati kwa walengwa na sisi kama kamati tutasimamia vema kugawa na kusimamia mtiririko wa ugawaji kwanzia ngazi ya wilaya,amkosi hadi kwa mkulima ili uzalishaji uweze kuongezeka, kwa yeyote atakaeenda kinyume na sheria hatutasita kumchukulia hatua stahiki”


Hata hivyo wilaya ya Kishapu msimu wa kilimo 2021/2022 haikufikia malengo ya kulima hekali 100,000 kutokana na upungufu wa mvua,upungufu wa vinyunyizi kwa wakulima hivyo kutokana na kampeini ya balozi wa pamba ya octoba 2022 wakulima wameendelea kupewa elimu ya kutosha kukabiliana na changamoto hizo huku wakikusudia ongezeko kubwa la wakulima wa pamba kwa msimu wa 2022/2023.

Balozi wa Pamba nchini  Tanzania Agrey Mwanri akizungumza kwenye Kikaoo 

Kikaoo cha Pamba kikiendelea


Katibu Tawala wilaya ya Kishapu Ndugu. Shadrack Kengese akizungumza kwenye Kikaoo 

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • DC MKUDE ATEMBELEA MGODI WA MWADUI KUJIONEA HATUA ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA BWAWA LA MAJI TOPE KUBOMOKA

    January 23, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPITISHA MPANGO WA BAJETISH BILIONI 39.4 KWAAJILI YA MAENDELEO

    January 20, 2023
  • KISHAPU YAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI

    January 12, 2023
  • BALOZI WA PAMBA NCHINI TANZANIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA

    January 09, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa