Baraza huru la kusikiliza malalamiko ya ukiukwaji wa haki za binadamu kwa wananchi waliopata madhira mbalimbali kwenye vijiji 12 vinavyouzunguka Mgodi wa Almasi wa Williamson WDL uliopo Mwadui limezinduliwa leo Mjini Shinyanga.
Baraza hilo limezinduliwa leo Novemba 29, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude kwa niaba ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe. Joseph Mkude amelitaka baraza hilo kufanya kazi kwa ufanisi na weledi ikiwa ni pamoja na kutenda haki kwa wananchi waliopatwa na madhira.
"Utaratibu uliotumika mpaka kufikia leo umekuwa wa wazi na tumekuwa tukieleweshwa ngazi moja hadi nyingine jambo ambalo ni jema na nila kiutu, hivyo tuoneshe uhalisia wa haki zinazotolewa pia kuwepo na uangalifu kwa walengwa wenyewe" amesema Mkude.
Akizungumza katika hafla hiyo Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamons Limited Richard Duffy, kampuni ambayo ni mwekezaji katika Mgodi wa Almasi wa Williamson Mwadui WDL ameshukuru na kupongeza juhudi mbalimbali zilizofanyika kufikia uzinduzi huo ambapo amesema baraza huru litafanya kazi kwa mafanikio makubwa.
"Napongeza juhudi mbalimbali ambazo zimefanyika katika kuunda baraza hili ambalo leo limezinduliwa hivyo naliiomba baraza hilo lifanye kazi kwa mafanikio makubwa" amesema Duffy.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza huru la Usuluhishi wa malalamiko Dr. Regemeleza Nshala amesema watapokea na kufanyia kazi malalamiko ya wanachi ya kuanzia mwaka 2009 hadi na kwamba jumla ya malalamiko 5575 yamesajiliwa na yataanza kusikilizwa mara moja
"Msingi Mkubwa utakaotuongoza ni utu na maridhiano, kwahiyo wale ambao wamedhurika kuanzia Februari 2009 hadi Mei 2021 malalamiko yao yatapokelewa ili yafanyiwe kazi, mpaka sasa tuna malalamiko zaidi 5,575 yaliyopokelewa na kusajiliwa na yote yanatakiwa yapitiwe na yahakikiwe" Amesema Dr. Nshala.
Nae Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe.Boniface Butondo amesema kuundwa kwa baraza hilo kutasaidia kuleta ushirikiano baina ya Mgodi na wananchi wanaouzunguka Mgodi huo.
Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya amewaomba viongozi mbalimbali kushirikiana na baraza hilo ili liweze kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamons Limited Richard Duffy akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza huru la kusikiliza malalamiko ya wananchi.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Petra Diamons Limited Richard Duffy akizungumza wakati wa uzinduzi wa baraza huru la kusikiliza malalamiko ya wananchi.
Mbunge wa jimbo la Kishapu Mhe.Boniface Butondo akipokea vitendea kazi vya baraza huru la kusikiliza malalamiko ya wananchi.
Mwenyekiti wa baraza huru akionyesha vitendea kazi vya baraza hiloMkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude na mtendaji mkuu wa kampuni yaPetra Diamons Limited Richard Duffy
wakipiga picha na wadau mbalimbali baada ya kuzindua Baraza huru.