• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPITISHA MPANGO WA BAJETISH BILIONI 39.4 KWAAJILI YA MAENDELEO

Posted on: January 20th, 2023

Kikao cha Baraza la madiwani wa halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga kimejadili na kupitisha mpango wa bajeti wa mwaka 2023/2024 Jumla ya Shilingi Bilioni 39.4

ambazo zitatumika katika kutekeleza miradi mbalimbali ya halmashauri hiyo.

ambapo bajeti ya Tarura ikiwa ni Shilingi zaidi ya bilioni 4.


Wakijadili ajenda ya kikao maalumu cha baraza la madiwani la kujadili na kupitisha mpango na bajeti ya mwaka 2023/2024 madiwani wa halmashauri hiyo  wamesema bajeti hiyo itatumike kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyoainishwa  na kuhakikisha inaondoa changamoto zote za halmashauri zilizopo.


Diwani wa kata ya Seke Bugoro Fednand Mpogomi amesema bajeti hiyo waliyoipitisha wanatakiwa wakaisimamie ipasavyo, pia amempongeza Meneja wa Tarura kwamba anafanya kazi yake kwa kujituma, lakini pia amesema kuna baadhi ya wakandarasi ni mizigo hawafanyi kazi zao kwa kiwango wanatakiwa wachunguzwe wasiendelee kupatiwa kazi.


"Bajeti yetu tumeipitisha leo, tunasisitiza wakuu wa idara na sisi wenyewe madiwani twendeni tukazisimamie  kikamilifu fedha zetu tulizozipitisha wenyewe  kwa ajili ya maendeleo ya halmashauri yetu na zikatatue changamoto za watu wetu ili kuhakikisha kero zilizopo zinaisha,"amesema Mpogomi.


"Pia naomba barabara ya Wishiteleja kwenda Mipa haimo kwenye bajeti hii naomba ihamishiwe kwenda Tanroad kutoka Tarura kwani ni barabara kubwa inaunganisha barabara ya lami kutoka Mwanza kwenda bariadi kupitia kijiji cha Mwakolongo inakutana na rami ya bariadi, kwa sababu tunaujenzi wa Reli bandari kavu, hivyo mizigo mingi itapitia pale,"ameomba Mpogomi.


Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri hiyo William Jijimya ambaye ni diwani wa kata ya Mondo ameagiza bajeti hiyo ikasimamowe na kuheshimiwa, ikafanye kazi inayotakiwa, madiwani wote na watendaji wakashirikiane kwa pamoja ili kuhakikisha kila mmoja anawajibika kwa kuzingatia idara yake.


"Bajeti hii imepitishwa kwa makusudi watumishi na madiwani simamieni ipasavyo lengo la serikali ni kuona mapato yanasimamiwa kwa asilimia 100, pia Rais wetu mama Samia Suluhu ametupa fedha nyingi sana  kwa ajili ya miradi  mbalimbali ya maendeleo,hivyo tunaomba asituchoke aendelee kutusaidia tuisimamie na tuhakikishe miradi yetu inakuwa ya kiwango zaidi,amesema Jijimya.


Katibu tawala wa wilaya ya Kishapu  Shadrack Kengese bajeti hii iliyopitishwa leo ikasimamiwe na miradi ya mkakati iliyopo ikasimamiwe na kukamilishwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na mapato ya ndani yakafikiwe, ili wilaya ya Kishapu ikawe ya mfano.


Aidha mkurugenzi wa halmashauri hiyo Johnson Emmanuel amesema bajeti hiyo iliyopitishwa wataisimamia ipasavyo ili kuhakikisha inatekeleza miradi ya maendeleo ya halmashauri ya Kishapu.


Diwani wa kata ya Kiloleli halmashauri ya Kishapu Edward Manyama akimsikiliza kwa makini mwenyekiti wa halmashauri hiyo akiwataka madiwani wakasimamie bajeti kikamilifu



Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese akizungumza kwenye kikao cha madiwani



Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM akizungumza kwenye kikao cha madiwani





Diwani akizungumza kwenye kikao

Diwani wa kata ya Seke bugolo Fednand Mpogomi akizungumza kwenye kikao cha madiwani



Madiwani wa viti maalumu kutoka wilaya ya Kishapu wakisikiliza kwa makini

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti

Madiwani wa halmashauri ya Kishapu wakiwa kwenye kikao cha maalumu cha mpango wa bajeti



Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu William Jijimya akizungumza kwenye kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya Mwaka  2022/2023

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • DC MKUDE ATEMBELEA MGODI WA MWADUI KUJIONEA HATUA ZILIZOCHUKULIWA BAADA YA BWAWA LA MAJI TOPE KUBOMOKA

    January 23, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI KISHAPU LAPITISHA MPANGO WA BAJETISH BILIONI 39.4 KWAAJILI YA MAENDELEO

    January 20, 2023
  • KISHAPU YAADHIMISHA MIAKA 59 YA MAPINDUZI ZANZIBAR KWA KUPANDA MITI

    January 12, 2023
  • BALOZI WA PAMBA NCHINI TANZANIA AWATAKA VIONGOZI KUSIMAMIA WAKULIMA WA ZAO LA PAMBA

    January 09, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa