Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu limekutana kwa ajili ya kukuwasilisha na kupokea taarifa za miradi ya maendeleo ya kata zake mbalimbali.
Katika kikao hicho cha kujadili taarifa za robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba, Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Mhe. Boniphace Butondo aliipongeza Kishapu kwa kupata hati safi kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu (CAG).
Mhe. Butondo ambaye pia ni diwani wa kata ya Lagana aliwataka madiwani waendelee kushikamana na kuwahudumia wananchi katika kata zao ili kueleta maendeleo katika halmashauri ya wilaya hiyo.
Alisema ni wajibu wao kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo katika kata zao sambamba na kuendelea kuwahamasisha kuhusu kilimo hususan cha mazao yanayostahimili ukame.
“Waheshimiwa tuwahudumie wananchi katika kata zetu na hasa ukizingatia hivi sasa Serikali inapiganaia katika kufufua zao la pamba katika wilaya yetu nasi tuwahamasishe kulima,” alisema.
Aliongeza kuwa katika kikao hicho Baraza linajipima wapi wamefikia katika miradi ya maendeleo na wapi wamekwama hivyo kuweza kutatua changamoto hizo na hatimaye kusonga mbele.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa