BARAZA LA MADIWANI WAPITISHA BAJETI YA BIL. 35/=
Baraza la Madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imefanya mkutano kwa ajili ya kujadili bajeti kwa mwaka wa fedha 2020/2021. Halmashauri imepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 35.5 ambapo kiasi cha shilingi bilioni 2.8 inatokana na mapato ya ndani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, Stephen Ndaki ambapo amesema miradi ya maemdeleo itakayotekelezwa katika mwaka wa fedha 2020/2021 imepengwa kiasi cha shilingi bilioni 6.5 ambapo mapato kutoka nyanzo vingine ikiwemo asasi za kiraia imetajwa kuwa ni shilingi bilioni 1.5.
“Mheshimiwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mpango wa bajati ya Halmashauri kwa mwaka ujao wa fedha wa 2020/2021 umeandaliwa kwa kuzingatia mwongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2020/2021, dira ya taifa ya maendeleo ya mwaka 2025, Mpango wa awamu ya pili wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini Tanzania (MKUKUTA II), Mpango wa Maendeleo ya Taifa wa Miaka Mitano, 2016/17-2020/2021, (FYDP II), Sheria ya Bajeti, SURA 439 pamoja na kanuni zake, Malengo Endelevu ya Maendeleo (SDGs)”. Alieleza Ndaki.
Katika mwaka ujao wa fedha halmashauri imeomba kuidhinishiwa kiasi cha shilingi bilioni 7.52 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo vipaumbele vitakuwa ni vile vilivyoibuliwa na wananchi.
Aidha katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2018/2019 halmashauri ilifanikiwa kutekeleza na kukamilisha shughuli mbalimbali kupitia idara na vitengo vyake.
Pia ilielezwa katika kipindi cha utekelezaji Julai hadi Desemba, 2019 palijitokeza changamoto kadhaa zikiwemo kucheleweshwa kupokea fedha na ruzuku ya matumizi mengineyo (OC) na miradi ya maendeleo toka serikali kuu na Wafadhili kutoka Hazina na wakati mwingine kupokea fedha pungufu au kutokupokea fadha hizo kabisa, upungufu wa mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani vya halmashauri, mabadiliko yatabia ya nchi kuathiri hali ya uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara hatimaye kupelekea tozo la ushuru wa mazao kutotimia lengo.
“Ili kuimaridsha ukusanyaji wa mapato na kufikia lengo tajwa, Halmashauri imeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya kulipa kodi ya majengo, kuendelea kuikumbusha Serikali kuleta fedha kwa wakati ili kutekeleza Mpango na Bajeti wa mwaka husika”alisema Ndaki wakati akiwasilisha bajeti.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa