• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

BARRICK YA UNGA MKONO UTAMADUNI MKOA WA SHINYANGA

Posted on: June 8th, 2022

Kaimu Meneja wa Mahusiano na Mazingira wa Barrick Bulyangh'ulu Zuwena Senkondo (kushoto) akiwa na wafanyakazi wenzake baada ya kupokea cheti cha shukrani kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema, (katikati) kutokana na kampuni hiyo kuunga mkono Tamasha la Utamaduni Mkoa 

Katika jitihada zake za kuunga mkono jitihada za Serikali za kukuza sekta ya utalii nchini, kampuni ya Barrick kupitia mgodi wa Bulyanhulu, imekuwa moja ya wadhamini wakuu wa Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga lililofanyika katika Kijiji cha Utamaduni wa Kabila la Wasukuma Butulwa – Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga.

Mbali na ufadhili kampuni iliwezesha ufungaji wa vifaa kwa ajili ya kuwawezesha wananchi waliohudhuria kwenye tamasha hilo kubwa kuweza kuona filamu maarufu ya kukuza utalii nchini ijulikanayo kama The Royal Tour, iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Tamasha hilo lilizinduliwa Juni 6,2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Juni 7,2022.

Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo, Mhe. Mjema amewapongeza na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la utamaduni ili kutii na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha kila Mkoa unaenzi na kudumisha tamaduni zao hivyo kuwakumbusha wananchi kuenzi tamaduni zao kama Rais Samia anavyosisitiza mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuenzi utamaduni zikiwemo mila na desturi.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Sophia Mjema wakati akifunga Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga Juni 7,2022. 

Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick katika Tamasha la Utamaduni mkoa wa Shinyanga.

Wananchi wakiwa kwenye Tamasha la Utamaduni mkoa wa Shinyanga.














Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • WANANCHI KISHAPU WATAKIWA KUPAZA SAUTI KUHUSU MMONYOKO WA MAADILI

    May 15, 2023
  • BARAZA LA MADIWANI LA MPONGEZA MKURUGENZI MTENDAJI KWA UKUSANYAJI MZURI WA MAPATO YA NDANI.

    May 10, 2023
  • WAZIRI JAFO APONGEZA MIRADI ILIYOTEKELEZWA

    May 06, 2023
  • RC MNDEME AMEAGIZA UJENZI WA BWAWA JIPYA LA MGODI WA ALMASI MWADUI LIJENGWE KWA KIWANGO BORA

    May 02, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa