Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Mhe, Joseph Mkude kwa Niaba ya Wananchi wa Wilaya ya Kishapu amepokea Pikipiki 15 aina ya Sunlg kutoka Bodi ya Pamba ambazo zitaenda kutumika na Maafisa Ugani.
Mhe, Mkude amepokea Pikipiki hizo leo katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kishapu na kuwaomba Maafisa ugani kwenda kutumia Pikipiki hizo kama ilivyokusudiwa kutumika.
“Maafisa Ugani nawaomba tukatumie Pikipiki hizi kama tulivyo jiwekea pikikipi hizi malengo yake ni kurahisisha usafiri kuwafikia wakulima na kuwaelimisha kwa kufata kanununi 10 bora za kilimo cha Pamba lakini pia kama tulivyojiwekea malengoya kutembelea angalau wakulima 20 wa kilimo cha Pamba lengo letu kuongeza uzalishaji wa Pamba Tani Laki moja (100000)” Mkuu wa Wilaya amesema.
Mkuu wa Wilaya baada ya kupokea Pikipiki hizo amemkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu ili aweze kuwakabidhi wataalamu (Maafisa Ugani).
Pia Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Ndg Emmanuel Johnson amekili kupoke Pikpiki 15 na kumwahidi Mkuu wa Wilaya atahakikisha Pikipiki hizo zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuwafikia wakulima wa Pamba katika maeneo yao.
“Mimi nichukue furusa hii kuishukuru Bodi ya Pamba kwa kutoa pikipiki hizi 15 kwajili ya Maafisa Ugani, Ndugu zangu nyie ni mashahidi Wananchi wetu bado wanalima Kilimo cha Mazoea na ili wabadilike ndiyo maana nyie Maafisa Ugani mpo, Na ili tuwawezeshe pia kiuchumi kama ilivyo sera ya Serikali ya kuwezesha kiuchumi lazima tuwasaidie walime Kilimo cha kisasa, na Wilaya yetu imepewa jukumu la kuzalisha Tani 100000 hivyo tujitahidi kuwafikia wakulima katika maeneo yao kama alivyoelekeza Mkuu wa Wilaya”. Mkurugunzi amesema
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa