Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mh. Nyabaganga Taraba Novemba 22, 2017 alizindua zoezi la upandaji miti kiwilaya ambapo aliwaongoza wananchi kupanda miti katika maeneo yao na maeneo mbalimbali.
Katika zoezi hilo ambalo linatarajiwa kuwa endelevu jumla ya miche 7,206 ilipandwa katika maeneo ya Mhunze, Kishapu, Isoso na Lubaga.
Mkuu huyo wa Wilaya aliambatana watmishi kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na watumishi kutoka taasisi zisizo za kiserikali wilayani humo.
Katika zoezi hilo wananchi walielekezwa njia bora za upandaji miche ya miti pamoja na umwagiliaji wa kisasa kwa njia ya matone ya maji kutoka kwenye chupa.
Zoezi la upandaji miti ni endelevu na linafanyika ili kusaidia kuhifadhi mazingira na kupunguza ukame katika maeneo ya wilaya hiyo kwa kuwezesha kunyesha kwa mvua.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa