Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Nyabaganga Taraba Jumamosi amewaongoza watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama kufanya mazoezi ya viungo.
Mazoezi hayo yaliambatana na kukimbia mchakamchaka yamefanyika ikiwa ni kuunga mkono kampeni aliyoizindua Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ili kuweka miili katika afya na kuepuka magonjwa yasiyoambukiza.
Iliagizwa kila Jumamosi ya pili ya mwezi watumishi wa taasisi za kiserikali nchi nzima kuwa na utaratibu wa kushiriki katika mazoezi hayo.
Mazoezi hayo yaliwashirikisha Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD), Emmanuel Gariyamoshi, askari Polisi na watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo kutoka idara mbalimbali.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa