• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Kishapu District Council
Kishapu District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Vitengo
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Ugavi na Manunuzi
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Uchaguzi
    • Idara
      • Fedha
      • Rasilimali watu
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
  • Machapisho
    • Fomu za kujinga na Kidato cha Tano
      • Shule ya Sekondari Kishapu
      • Shule ya Sekondari Shinyanga
    • Mpango wa bajeti wa mwaka 2021/2022
    • MATANGAZO
  • Madiwani

DC MKUDE AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAOFISA UGANI NA WATENDAJI WA KATA

Posted on: March 9th, 2023

MAOFISA Ugani na Watendaji wa Kata Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, wamepewa vitendea kazi Pikipiki, ambazo watazitumia kwenye shughuli za Kiserikali.

Zoezi la kukabidhi Pikipiki hizo limefanyika leo Machi 9, 2023 katika Ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ilikuona namna Serikali Chini ya Rais Samia inavyotekeleza Ilani ya CCM kwa vitendo.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza wakati wa kukabidhi Pikipiki hizo, amewataka Maofisa Ugani kuwa Pikipiki hizo zikatumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa ikiwamo kuleta tija kwenye Sekta ya Kilimo.


“Maofisa Ugani leo tumewakabidhi vitendea kazi Pikipiki hizi hatuta tegemea kusikia Mkulima ambaye hajatembelewa na kupewa elimu ya Kilimo cha kisasa, tunataka tuone mabadiliko kwenye Sekta ya Kilimo sababu hakuna visingizio tena vya usafiri, Rais Samia ametatua tatizo hilo na kujali watumishi wake hivyo msimwangushe,”amesema Mkude.


Aidha, amewataka pia Watendaji wa Kata kwamba Pikipiki ambazo wamepewa wakazitumie vizuri ikiwamo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato.


Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, amewataka Maofisa Ugani pamoja na Watendaji wa Kata, wanapokuwa wakiendesha Pikipiki hizo wazingatia pia matumizi ya usafiri wa Serikali na siyo kukutwa nazo mida ya usiku zikiwa bar.


Pia amemuagiza Mkuu wa Polisi wilaya ya Kishapu, kuwa Watumishi hao kabla ya kuanza matumizi ya Pikipiki hizo, wapewa kwanza mafunzo ya Sheria za Usalama Barabarani, huku akiwataka wale ambao hawana Lesseni wazikate.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, amesema Wizara ya Kilimo imetoa Pikipiki 39 kwa Maofisa Ugani wilayani humo, na Pikipiki Nne za Watendaji wa Kata zimetolewa na Ofisi ya Rais (TAMISEM), huku Pikipiki nyingine 10 ambazo zilinunuliwa na Halmashauri wamewapatia pia Watendaji wa Kata.


Nao baadhi ya Maofisa Ugani akiwamo Tito Nzungu wa Kata ya Ndoleleji, ameipongeza Serikali kwa kuwapatia vitendea kazi na kuahidi Pikipiki hizo watazitumia kwa madhumuni yaliyokusudiwa, na kuleta tija kwenye sekta ya kilimo, kwa kuwatembelea wakulima muda wote na kutoa elimu ya kilimo cha kisasa na kuongeza uzalishaji.

Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MFAMASIA December 14, 2021
  • RATIBA YA UFANYAJI MAZOEZI KWA KILA WIKI August 16, 2021
  • Tazama yote

Habari Mpya

  • MKUU WA WILAYA YA KISHAPU AFANYA ZIARA YA KUSHITUKIZA SEKE- IDIDI

    March 22, 2023
  • DC MKUDE ATOA MAELEKEZO ULIPAJI FIDIA WAHANGA WA TOPE LA MGODI WA MWADUI

    March 21, 2023
  • DC MKUDE AKABIDHI PIKIPIKI KWA MAOFISA UGANI NA WATENDAJI WA KATA

    March 09, 2023
  • SHULE YA SEKONDARI BUSIYA YA PATA MSAADA WA SARUJI MIFUKO 140

    March 08, 2023
  • Tazama yote

Video

EGA ANNOUNCIMENT
Video zaidi

Viunganishi cha Haraka

  • fomu mbalimbali
  • Dira na Dhima ya Halmashauri

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Kuu ya Serikali
  • Tovuti ya Ofisi ya Rais Ikulu
  • Tovuti ya Utumishi
  • Tovuti ya OR-TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu
  • Tovuti ya Idara ya Habari Maelezo

Watazamaji mbalimbali Duniani

world map hits counter

Idadi ya wasomaji

free HitCounter

Mwonekano wa Ramani

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Wilaya Kishapu

    Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU

    Simu ya mezani: +255282770020

    Simu:

    Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa