Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga ametembelea kijiji cha Idukilo na kuzungumza na wananchi kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo.
Katika ziara hiyo Magoiga aliambatana na timu ya watalaamu wakiwemo Afisa Elimu Msingi, Sostenes Mbwilo, Afisa Mipango, Mang’era Mang’era na Afisa Elimu Ufundi, Moshi Balele.
Aliwahimiza wananchi kijijini hapo kwenye kata ya Idukilo kushirikiana kwa pamoja katika kusimama miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali kupitia fedha zinazotolewa.
Mkurugenzi huyo alisema wananchi wana wajibu wa kuchangia shughuli za ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo vyumba vya madarasa na nyumba za walimu kwa njia mbalimbali.
“Kamati ya shule, serikali ya kijiji na watalaamu kutoka wilayani wote mnapaswa kushirikiana kwa pamoja katika kusimamia shughuli za miradi zinazotekelezwa katika kijiji chenu,” alisema.
Katika mkutano huo wa hadhara pia mkurugenzi ikiwa ni mojawapo wa utaratibu aliojiwekea, alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa wananchi kijijini hapo.
Halmashauri ya Wilaya Kishapu
Anwani ya Posta: S.L.P. 1288 KISHAPU
Simu ya mezani: +255282770020
Simu:
Barua pepe: info@kishapudc.go.tz/ded.kishapudc@shinyanga.go.tz
Hakimiliki © 2016 Halmashauri ya wilaya ya Kishapu. Haki zote zimehifadhiwa